Pep Guardiola na Simulizi ya Sir Alex Ferguson - EDUSPORTSTZ

Latest

Pep Guardiola na Simulizi ya Sir Alex Ferguson
Bado macho yangu ni makavu! Usiku wa saa nane wakati sauti ya bundi na milio ya wadudu usiku, naendelea kupitia kitabu cha ANOTHER WAY OF WINNING cha Pep Guardiola

Asubuhi moja ya kijua cha kiangazi Septemba 10,2010 kwenye majengo ya shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) pembezoni mwa Ziwa Geneva, Uswisi! Kwenye kikao cha mwaka cha Makocha, Pep alipata bahati kubwa

Licha ya kuwa alimfunga Ferguson na United yake fainali ya UEFA 2009 Ila kwake alimuhusudu sana Fergie na ni kawaida yake kupenda Makocha wazee kama ilivyo Marcelo Bielsa ambae yeye kwake ndio Godfather

Pep yeye akiwa Kijana Mdogo bado aliona ndio muda sahihi wa kukaa na Sir Alex na kujadili mpira, wakiwa wameketi, Pep akawa anamsikiliza Fergie akimpa tactical trends za Ulaya nzima, maana Babu alikuwa Mtaalam mno wa mifumo

Pep aliendelea kuketi kama Kijana mtiifu mwenye ndoto kubwa, akimsikiliza Babu akipangua vihendo kuanzia kwa Arrigo Sacchi, Bobby na mafundi wengi wa soka! Kazi ya Pep ilikuwa ni kuongeza kahawa tu kwenye kikombe cha Fergie

Kumbuka ni Pep Guardiola huyo ambaye tayari ametwaa ubingwa wa Ulaya mbele ya Fergie na United yake ila bado anatumia muda wake kujifunza, haringi kabisa maana kila muda kwake yeye ni football tu

Kwakuwa Nyon iligubikwa na Makocha wakubwa wengi, Pep ndio kwanza alikuwa anachipukia hivyo alionekana Mtoto pale! Alikuwepo Mourinho alimtoa Pep Nusu UEFA 2010, Carlo Ancelotti, Claudio Ranieri, Babu Fergie na wengine

Wakati wapo Makocha wakubwa wamejikusanya wanajadili kabla ya kurudi kikaoni, Pep akajitoa pale na kujisogeza pembeni Kwakuwa alikuwa anajiona mdogo na hawezi kuongea kitu mbele ya Magwiji😄

Wakati Pep kajitenga pembeni, Jose Mourinho alimuona, ikabidi Mourinho atoke kwenye lile kundi na kwenda kupiga nae stori maana alikuwa mwenyewe kajitenga, wana kisa chao hawa kumbuka😄

ITAENDELEA....

#MOROGORO
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz