elru87tYGBGEm Manara, Bumbuli Wamewakosea Wadhamini Yanga Sakata la Manara Kutoa Nembo ya Chupa ya Maji - EDUSPORTSTZ

Latest

Manara, Bumbuli Wamewakosea Wadhamini Yanga Sakata la Manara Kutoa Nembo ya Chupa ya MajiWakati Haji Manara ana mgororo na uongozi wa Simba niliandika kuwa ni wakati sahihi wa Manara kuondoka klabuni hapo, kwani mazingira yalionyesha wazi haitawezekana kurudu nyuma.

Haji alifanya kazi kubwa akiwa Simba, licha ya kulipwa mshahara ambao alieleza kuwa hauendani na kazi yake, lakini upande wa pili alitumia ‘platform’ ya Simba kuingiza fedha nyingi, hiyo ilikuwa ni ujanja wa akili yake katika ‘kujiongeza’.

Ukurasa ukafungwa, sasa Manara yupo Yanga, licha ya kuwa ni mwajiriwa wa klabu hiyo lakini nyuma ya pazia ana mikataba binafsi.

Jumatano Septemba 8, 2021, katika mkutano rasmi wa waandishi wa habari, @hajismanara alionekana akitoa mezani maji ya Kampuni ya Afya, akasikika akihoji juu ya wadhamini hao wa Yanga, ni kina nani? Wanalipa shilingi ngapi na mkataba wao unaisha lini?

Aliuliza maswali hayo kwa sauti ndogo wakati akizungumza na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan #Bumbuli.

Kwa uzoefu wa Manara alionao, akiwa anajua kuna kamera na vipaza sauti mbele yake, hata kama bado walikuwa hawajaanza rasmi mkutano wa huo, siamini kama alizungumza hayo maneno kwa bahati mbaya hata kama sauti ilikuwa chini.

Kitendo cha Manara kutoa mezani maji ya mdhamini wa klabu, kisha kubandua lebo, kusikika akisema huo ni mtihani kwake kwa kuwa ana wadhamini wengine binafsi ambao ni washindani wa mdhamini wa Yanga, halikuwa jambo la kiungwana.

Mtaani kuna hoja kuwa mbona Cristiano Ronaldo na Paul Pogba walitoa bidhaa za mdhamini mbele ya mkutano wa waandishi.

Ufafanuzi upo hivi, Ronaldo na Pogba walitoa kinywaji cha wadhamini wa michuano shiriki walipokuwa Euro na siyo wadhamini wa klabu zao.

Lionel Messi na Ronaldo wana mikataba binafsi na makampuni kama Nike au Adidas lakini klabu zao zimekuwa zikidhaminiwa na kampuni tofauti za zile za binafsi lakini hawajawahi kukataa kutangaza kampuni shindani wakiwa katika majukumu ya klabu.

Kibaya zaidi Bumbuli anasikika akimwambia Manara hao Afya ‘WANATOA HELA YA KAWAIDA.’

Mkutano ulikuwa ni wa Klabu ya Yanga, wadhamini ni wa Yanga, Haji Manara ni muajiriwa wa Yanga kisha, hakutakiwa kutoa chupa wala kubandua lebo ya mdhamini kisha tu ana mdhamini wake binafsi.

Na @johnharamba  
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz