Afande Msemwa Aanza Kutoa Ushahidi Kesi ya Mbowe - EDUSPORTSTZ

Latest

Afande Msemwa Aanza Kutoa Ushahidi Kesi ya Mbowe

SHAHIDi wa tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameanza kutoa ushahidi wake.

Shahidi huyo askari polisi mwenye namba H 4323 Constable Msemwa kutoka Kituo Cha Polisi Oysterbay, ameanza kutoa ushahidi wake leo, Septemba 20, 2021 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Shahidi huyo anaongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, mbele ye Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza shauri hilo.

Msemwa anatoa ushahidi wake, baada ya shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo, Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Mahita Mahita kumaliza kutoa ushahidi wake na kisha kuhojiwa na mawakili wa upande wa utetezi kuhusiana na ushahidi alioutoa mahakamani hapo, kuhusiana na kielelezo kinachobishaniwa na upande wa utetezi.

Mbowe na mwenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz