Wasanii wa Bongo Kuna la Kujifunza Kutoka Kwa Burna Boy, Tuache Porojo - EDUSPORTSTZ

Latest

Wasanii wa Bongo Kuna la Kujifunza Kutoka Kwa Burna Boy, Tuache PorojoUsiku wa jana msanii @burnaboygram alikuwa na show yake nchini uingereza kwenye Arena maarufu na yenye hadhi ya juu nchini humo,The 02 Arena ambayo inaingiza watu Elfu 20 pekee na alifanikiwa kumaliza tiketi kabla ya show na ndani ya muda mchache toka atangaze kupatikana kwa tiketi ya show hiyo.

Si jambo tena kwa wasanii wa Nigeria kwenye vitu kama hivi kwasasa lakini kubwa aliloonyesha Burna Boy ni Love kwa wasanii wachanga wa nchini mwake.

Kwenye stage walipanda wasanii @omah_lay ,@heisrema na @rugerofficial katika utangulizi wa show hiyo na wote hawa ni kutoka Nigeria, Burna Boy aliwapandisha flight machalii hadi UK, wakafanya show na akawalipa japo ilikuwa ni ishu ya kuwafungulia mipaka kwenye soko la nje ya Afrika.

Burna Boy hana Record Label na hana maslahi yoyote kwa wasanii hawa,na hili libaki kuwa somo kwa wasanii wa bongo na sekta nyingine,kuwa na love ya aina hii ni kila kitu.kupitia insta Story yake Burna ameandika..

"nimemaliza tiketi nikiwa mwenyewe,kwa bei niliyoitaka na namna nilivyotaka,usiongee sana,onyesha vitendo". Hatuelewi kamlenga nani ila hata bongo wapo wenye kuvimba.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz