Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumsimamisha kazi Mwalimu Omary Kwesiga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Arusha baada ya kuonekana wakifanya igizo katika zoezi la uchomaji wa chanjo ya COVID-19.
Aidha Waziri Ummy ameagiza Afisa Muuguzi Msaidizi katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha Scolastica Kanje, aliyekuwa akishirikiana naye katika igizo hilo la uchomaji wa chanjo hiyo kupelekwa kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga kwa hatua zaidi, ambapo Baraza hilo limeagiza muuguzi huyo asimamishwe kazi kwa miezi mitatu.
Hatua hiyo imekuja baada ya video clip kusambaa mitandaoni ikionesha wawili hao kufanya igizo hilo.
No comments:
Post a Comment