Steve ATOA Neno ISHU YA Manara 'Kumbe Huna Lolote ni Mikwala tu' - EDUSPORTSTZ

Latest

Steve ATOA Neno ISHU YA Manara 'Kumbe Huna Lolote ni Mikwala tu'


BUSARA ZA @STEVENYERERE2

Nimetumia Masaa 24 kurudia kuskiliza unaongea nini jana @hajismanara Yawezekana wapo walio kuelewa na wasio kulewa yapo maswali mengi mtaani kwa nini kama alikuwa anafanyiwa haya yote asinge sema siku zote hizo,Aje aseme leo, Na wapo wanaosema kama alikuwa anafanyiwa hayo kwa nini asinge jiuzuru muda, Ila wanasahau Pamoja na hayo yote uliyokuwa unapitia Uliamua kubaki na mapenzi ya damu kwa Timu yako, Matatizo yanaweza kukufanya kuwa imara zaidi kama utachanganya na mapenzi, Pamoja na yote Mimi naona ulisimama kwenye mapenzi na Timu yako bila kujali unapitia changamoto gani, Nikaendelea tena kuskiliza Nikawa nipo Darasani Kumbe siku zote hizo mbwembwe zote zile kujigamba kujimwambafayi unatutisha na majina ya magari kumbe hata tiketi ulikuwa upewi, Nimejifunza kitu kutokana na press yako jana Sio kila mwenye cheo ana maamuzi, Haiwezekani mikwala yote ile na tiketi unajilipia na ulivo kuwa unatutisha doooo kumbe huna lolote ni mikwala tu kweli mimi nimekalili maisha yale ya zamani kila mwenye kitambi Tajiri, Kikubwa Jana umetoa yale yote ya moyoni mwako, Umetoa kinyongo chako, na vizuri kutoa kinacho kuumiza maana maisha ni mafupi sana, Ushauri wangu sasa Tuangalie soka letu kwa sasa, Hizi porojo zifungwe maana hazisaidii Soka yetu na timu zetu, Nitashangaaa sana Kama wapo watu wanajipanga kuendeleza Mambo haya,Staki kuamini kama kutatokea majibizano au ile kauli ya tunajibu mashambulizi au kupelekana mahakamani kwa kunichafua nadhani tujue mipira ina mambo mengi sana .Maana inagusa hisia za watu, kwa wale wa kiki naomba huu mjadala ufungwe maana wapo watu nao wataona hapa hapa ndio njia ya kujulikana na kujipendekeza, Wapo chawa nao wapo kazini muda huu, Kwa maslahi ya soka letu tufunge mjadala tumtangulize Mungu mbele, Tufunge mjadala UJUMBE WANGU LEO,, MAUMIVU NI YA MUDA MFUPI, LAKINI UKIRUDI NYUMA YATAKUSUMBUA MILELE,..

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz