Mtaka "Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mtaka "Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19"

 


Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kwa sababu hali si nzuri mkoani humo.

Ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 3, 2021 wakati akizungumza na askari wa usalama wa barabarani na viongozi wa masoko wa mkoa wa Dodoma.

Amewataka askari hao, viongozi wa masoko na wafanyabiashara kuhakikisha wanachukua hatua za kujikinga katika maeneo yao kwa kuvaa barakoa na kunawa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

Pia amewataka askari wa usalama wa barabarani kuhakikisha watu wote wanakaa kwenye viti (level seat) kwenye daladala na bajaji na kwenye bodaboda kuhakikisha hawabebi abiria zaidi ya mmoja.

Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Boniface Mbao amesema watakapotoka katika kikao hicho wataenda kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa elimu na ikibidi kwa ukali, ili kuhakikisha abiria wanakaa katika viti kwenye mabasi ya abiria.

Amesema hakuna gari litakalopita kwenye mkoa huu likiwa limejaza zaidi ya abiria waliokaa kwenye viti





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz