Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitangaza siku ya tarehe 5 Agosti mwaka huu kama siku ya kupinga kukamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe .
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Chama hicho ,John Mnyika amedai kilichofanyika kwa Mwenyekiti huyo ni uendelezaji wa ukandamizaji wa demokrasia nchini.
“Mbowe alikuwa kwenye kazi ya kutetea Katiba Mpya ,Mbowe alikuwa kwenye kazi ya ujenzi wa chama ,Mwenyekiti Freeman Mbowe anapaswa kuachiwa huru mara moja” –John Mnyika
“Chama kimeacha uhuru kwa wananchi , wanachama na viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali waweze kuandaa matukio ya kupinga mashtaka ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na matukio ya kudai Katiba mpya katika siku hiyo “ John Mnyika
Chama hicho pia kimesema baada ya tarehe hiyo kitapanga upya ratiba za makongamano kwa ajili ya Katiba Mpya kwa nchi nzima.
No comments:
Post a Comment