Mfanyabiashara Ndama Ahukumiwa Kulipa Dola 75,000 - EDUSPORTSTZ

Latest

Mfanyabiashara Ndama Ahukumiwa Kulipa Dola 75,000

 


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mfanyabiashara maarufu nchini,  Ndama Shabani ‘Ndama mtoto wa Ng'ombe’ na mwenzake Yusuph Yusuph kulipa fidia ya dola za kimarekani 75,000 kwa malalamikaji Emanuel Motilhathedi baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia dola za kimarekani 150, 000 kutoka kwa mlalamikaji huyo ambaye ni raia wa Botswana kwa madai kuwa wangemuuzia kilo 500 za dhahabu lakini hawakufanya hivyo.

Hukumu hiyo imetolewa leo,  Jumatatu Agosti 2, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya baada ya washtakiwa hao kukiri mashtaka, kupitia majadiliano baina yao na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP).

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz