Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa Akwepa Mtego wa Polisi - EDUSPORTSTZ

Latest

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa Akwepa Mtego wa Polisi


Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa ameingia Bungeni Majira ya saa Moja Asubuhi kutii wito wa kwenda mbele ya kamati ya Bunge ya haki Maadili na madaraka ya Bunge akiwa peke yake bila kusindikizwa na Polisi.

Siku ya Jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo aliomba kibali cha kukamatwa kwa Mbunge huyo ili kufikishwa mbele ya kamati kutokana na kukaidi kufika katika siku aliyopangiwa.

Baada ya kufika Bungeni Jerry alielekea Jengo la Utawala na baadae ilipofika Majira ya saa Nne akaingia kwenye Ukumbi wa kamati ya Maadili kabla ya Mwenyekiti na wajumbe wake kuingia.

Alipoingia mwenyekiti wa kamati hiyo Emanuel Mwakasaka akaamuru mbunge huyo atoke nje ya Ukumbi na Asubiri kuitwa kama utaratibu unavyosema.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz