Kajala Awachana Wanaoingilia Maisha Make - EDUSPORTSTZ

Latest

Kajala Awachana Wanaoingilia Maisha Make





MUIGIZAJI wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka na kusema kuwa amechoka na tabia za watu kuendelea kufuatilia maisha yake binafsi.


Kajala amesema kuwa, baadhi ya watu wanapoamua kumsema kila kukicha kwenye mitandao yeye na mtoto wake, Paula, basi wajue wanazidi kumuongezea siku za kuishi hapa duniani.

 

Alisema kuwa, hii ni kwa sababu wanaofanya hivyo hawahangaiki na vitu vyao vinavyowahusu, badala yake wako bize na mambo yake na mwanawe.



Kajala amesema kuwa, anawashangaa watu wengi wameacha kazi zao zinazowahusu za kila siku badala yake wako kwenye mitandano kumtukana yeye na mtoto wake, jambo ambalo linamkwaza.

 

Kajala amekuwa akiandamwa juu ya malezi ya mwanawe, Paula wakimtuhumu kumuingiza kwenye mambo ya kikubwa angali bado na umri mdogo wa miaka 19, tayari yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny.







Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz