Dk. Mollel: Tutamshugulikia Mch. Gwajima - EDUSPORTSTZ

Latest

Dk. Mollel: Tutamshugulikia Mch. GwajimaNaibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Siha, Mhe. Dkt. Godwin Mollel amemtaka Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kujitafakari juu ya madhara yatakayo wakuta wananchi kutokana na upotoshaji anaoendelea kuufanya na kuongeza kuwa hawezi kupingana na Serikali na hana uthibitisho wa kisayansi.

 

“Gwajima amevuka mipaka, anapotosha Taifa, hawezi kupingana na serikali na hana uthibitisho wa kisayansi, anasema mtu akichanjwa kuna vitu vinaingizwa mwilini ili mtu afe baada ya miaka miwili ama kumi, tutamuita athibitishe hili, akishindwa tutamshughulikia.

 

“Nimekuja kumuonya nikiwa kama mwana sayansi, ili ajue kwamba ametukanyaga sehemu, Gwajima anajua ukweli lakini ameamua kucheza ligi, tunamuonya tunataka awe na uthibitisho wa Kisayansi kwa kile anachosema kuhusu Chanjo ya Corona.

 

“Tumetumia nguvu nyingi sana kumuelimisha (Askofu Gwajima), tunataka tuthibitishiane kwamba sisi na yeye nani anataka kuiangamiza nchi, tujue nani anataka kuilinda nchi,” amesema Dk. Mollel
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz