KATIKA moja ya simulizi alizopitia msanii machachari na malkia wa Bongofleva, Zuhura Omar maarufu kama Zuchu ni kipigo alichokipata kutoka kwa kaka yake Suma Kopa ambao wote mama yao ni malkia wa taarabu, Hadija Kopa.
Zuchu ambaye sasa anatamba vilivyo na wimbo wake wa nyumba ndogo ambao unakwenda kwa mahadhi ya singeli, inadaiwa alichapwa na ufagio wa chelewa kiasi cha kupelekwa hospitali kutolewa baadhi ya vijiti vya ufagio huo vilivyokuwa vimeingia kwenye ngozi.
MKASA ULIKUWA HIVI
Akisimulia kwa kina mkasa huo katika moja ya mahojiano yake wiki iliyopita, Suma Kopa ambaye ni kaka yake wa pili Zuchu baada Omar aliyefariki kwa ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita, alisema tukio hilo la kumchapa mdogo wake kamwe hatolisahau.
“Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa navuta bangi sana, Mungu asinirejeshe huko, nilikuwa teja lakini wa bangi sio unga, nilikuwa nikiamka ni kuvuta bangi, akili zangu ilikuwa ukizingua nakuzingua.
“Basi kwa kuwa mimi makazi yangu toka utotoni ni Zanzibar, nilikuja Bara kwa kwa mama huko Mwananyamala… nikaenda kule nyuma kuvuta bangi na washkaji, niliporejea nyumbani kwa mama, sikuelewa mambo yanayoendelea maana sikuona msosi na mambo mengine.
“Nilipoulizia hapa vipi masuala ya msosi, badala ya kujibiwa mfanyakazi, akajibu Zuhura ‘Zuchu’ jibu ambalo lilinikera. Ingawa si kwa ubaya lakini nikamind nikamshika na kumtia fimbo sana zile chelewa hadi akaenda hospitali kutolewa zile chelewa za ufagio.
“Kiufupi nilikuwa mgonjwa na nilikuwa nampiga kama msela mwenzangu, ila si kwa ubaya… kwa sababu nampenda sana, ndiye mimi niliyemlea utotoni wakati mama akiwa kwenye mizunguko ya kutafuta pesa.
“Kaka Omar alikuwa mkubwa kwa hiyo mimi ndio mdogo ambaye nilibaki na mtoto nyumbani kwa muda mrefu.
“Pamoja na mapito hayo, hadi sasa nahisi bado Zuchu ananiogopa kati ya kaka zake wote, ila tu nimwambie ule ulikuwa ugonjwa tu, na sasa sina kinyongo naye chochote,” alimaliza Suma.
GPL
Post a Comment