WATOTO wawili wamefariki dunia na wengine 15 wamenusurika kifo baada ya kula chakula ambacho kinadhaniwa kuwa na sumu katika sherehe ya harusi.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, wakati akizungumza na waandishi wa habari, amewataja waliofariki kuwa ni Manyirizu Joseph (6) na Bertha Mateso (5) ambao wote ni wakazi wa Ikobe wilayani Mbogwe.
Kamanda Mwaibambe amesema watoto hao na wengine waliojeruhiwa walikula mabaki ya chakula (kiporo) ambacho ni wali na nyama ya kondo na kuanza kutapika pamoja na kuharisha.
Aidha, Kamanda huyo amesema hali ya manusura wanaendelea na matibabu katika kituo cha afya Iboya wilayani Mbogwe mkoani humo na hali zao zinaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment