Watu saba mbaroni tukio la la moto sekondari ya Geita - EDUSPORTSTZ

Latest

Watu saba mbaroni tukio la la moto sekondari ya Geita

Watu saba wanashikiliwa kwa Mahojiano na jeshi la polisi Mkoani geita kufuatia Matukio mfululizo ya Moto uliounguza Madarasa na vifaa vya wanafunzi katika shule ya sekondari ya geita GESECO Iliyopo mkoani humo
Akizungumza wakati akikabidhi baadhi ya vifaa vya wanafunzi vilivyoathirika kwa la janga la moto huo shuleni apo  mkuu wa mkoa wa geita  Rosemary Senyamule amesema wanaoshikiliwa ni wanafunzi watatu wa shule hiyo pamoja walinzi wanne waliokuwa wanalinda shule hiyo

Sambamba na serikali ya mkoa wa geita kufanikiwa kukabidhi magodoro 240 , masanduku 240 pamoja na madaftari kwa wanafunzi wa shule hiyo RC Rosemary Senyamule amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusadia ukarabati wa majengo yaliharibiwa vibaya  na janga hilo la moto
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz