Wanafunzi 10 bora masomo ya sayansi kidato cha sita 2021 hawa hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Wanafunzi 10 bora masomo ya sayansi kidato cha sita 2021 hawa hapa

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2021 na kutaja wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi.


Akizungumza leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amemtaja Perucy Astus Mussiba kutoka shule ya Canossa, Dar es Salaam kuwa kinara wa matokeo hayo, katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.Nafasi ya pili imechukuliwa na Donard Rulers Mosile kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri (Arusha) kutoka PCB. Cretus Amos Mihayo kutoka Tabora  Boys (Tabora) PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Ismail Mtumwa kutoka Kibaha Sekondari(Pwani) PCM aliyeshika nafasi ya nne.Nafasi ya tano imechukuliwa na Olais Julius Mollel kutoka Kisimiri (Arusha) PCM akifuatiwa na Geofrey Sanga alieshika nafasi ya sita kutoka Tabora  Boys (Tabora) PCM.Anord Msanga kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM akichukuwa nafasi ya saba Caroline Mpale amechukuwa nafasi ya nane  kutoka Canossa Sekondari( Dar es Salaam) akichukuwa mchepuo wa PCM.Nafasi ya tisa na kumi imechuukuliwa na wanafunzi kutoka Feza Boys (Dar es Salaam) PCM John Bugeraha aliyechukuwa nafasi ya tisa na Harry Mshana aliyechukuwa nafasi ya kumi.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz