Uongozi wa Simba wamzawadia gari Musa Mgosi - EDUSPORTSTZ

Latest

Uongozi wa Simba wamzawadia gari Musa Mgosi

Uongozi wa Klabu ya Simba umemzawadia kocha mkuu wa timu ya wanawake ya klabu hiyo Mussa Hassan Mgosi kwa kuiongoza timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya wanawake kwa mara ya pili mfululizo.
Musa baada ya kupewa zawadi hiyo ya gari kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika‘Asante Simba Sports Club kwa zawadi ya Gari ila makabidhiano naomba yawe siku ile ya mechi ya SIMBA S.c wakikabidhiwa kombe la V.P.L hii itasaidia kwa wachezaji kuiga maadili ya kuitumikia Simba kwa nidhamu na uadilifu- Musa Hassan Mgosi

‘Pia nichukue fursa hii kuwashukuru TFF na Benchi la TWIGA STARS na UONGOZI wa SIMBA kwa kufanikisha mechi ya jana kwa jili Simba Queens KUPATA MECHI ya kujipima na kuiangalia nini kifanyike kabla ya mchuano ya kimataifa kuanza matokeo ni kitu kingine’- Musa Hassan Mgosi

‘Ila naamini kwa ukanda wa CECAFA NGAZI ya vilabu hakuna team bora yenye cream ya wachezaji bora kama team ya Taifa ambayo tumecheza jana hivyo niendelee kuomba tupate kucheza mechi hiyo kwa mara nyingine zaidi kutakapo kuwa na nafasi ya hilo lengo ni kuijenga Simba Queens kwakuwa wana jukumu la kitaifa na team TAIFA TWIGA STARS wanajukumu la TAIFA’- Musa Hassan Mgosi


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz