Tanzania Yairudisha Selous Kwenye Urithi Wa Dunia - EDUSPORTSTZ

Latest

Tanzania Yairudisha Selous Kwenye Urithi Wa Dunia



Happy Lazaro,Arusha
Arusha.Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Dk.Allan Kijazi amesema serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa shirika la umoja wa mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) waliopo hapa nchini wamefanikiwa kuirudisha Poli la akiba la selous ili iendelee kuwepo kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia .

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichoendeshwa kwa njia ya mtandao na kuhudhuriwa na nchi wanachama  21  Dk Kijazi amesema taarifa zilizokuwa zimetumika kutaka selous iondolewa kwenye orodha zilikuwa sio sahihi kwakuwa zilikuwa zimetegemea  kusikia na sio kupata taarifa kamili kutoka kwa nchi husika.


“Kama ambavyo tuliripoti wakati  wa mkutano wa unesco ulipoanza kulikuwa na mapendekezo ya selous kuondolewa kwenye  orodha ya maeneo ya urithi wa dunia  sisi na wataalamu tumekaa na kuona taarifa zilizotumika si sahihi na zilikuwa na uongo mwingi  “amesema .


Dk Kijazi ameongeza kuwa, mapendekezo ambayo yalikuwa yametolewa na IUCN pamoja na World heritage cental ambayo yalitumika  kuishauri UNESCO kuiondoa selous yalikuwa hayajafuata utaratibu kwa kuwa walikuwa hawajashirikishwa  kitu ambacho ni tofauti na miongozo walikubaliana kwenye kuchagua na kusimamia maeneo hayo .

 
“Wataalamu wamefanya kazi kubwa kueleza ukweli kuhusu hali ilivyo na kuziambia nchi  wanachama ishirini na moja ambazo zinapiga kula kuwa utaratibu umekosea na taarifa zilizotolewa sio sahihi   kwahiyo selous iendelee kubaki na kuwaomba IUCN pamoja na world heritage cental kukusanya taarifa zenye usahihi na sio za kupotosha dunia” ameongeza .


Kwa upande wake Profesa Hamisi Malebo ambaye ni  Katibu mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO  kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema taarifa iliyokuwa imetolewa ilikuwa imetiwa chumvi kwakuwa walikuwa wamesema selous ilikuwa imepoteza sifa kwa kuwa wamefyeka miti yote na kusababisha uharibifu kitu ambacho sio kweli kwakuwa eneo lililokuwa limefyekwa ni dogo sana .


“Walisema tumefyeka miti yote kwaajili ya kujenga bwawa akati ni sehemu chache sana iliyofyekwa miti  na pia walise  tembo wamepungua wakati tukiangalia tembo wamezaliana sana katika pori hili kwaiyo tunashukuru kuwa tumeweza kuionesha dunia ukweli wote ambao ulipindishwa na mataifa wameelewa na kupingana na IUCN katika taarifa waliyokuwa wameotoa” amesema 


Malebo ameongeza kuwa ,kazi ya kitaalamu huwa ni kuchambua vile vitu ambavyo sio vya kweli kwa kuwa IUCN ni wataalamu washauri wa unesco ni rahisi kukukandamiza usipokuwa makini kwa kuchambua vitu ambavyo ni muhimu .


Naye Evelin Swai ambaye ni Mratibu wa masuala ya unesco kutoka wizarani amewashukuru wataalamu wote waliosaidia kuitetea selous kurudishwa kwenye maeneo ya urithi wa dunia na kusema kuwa ujenzi wa bwawa haukuwa tishio kwenye hifadhi hiyo na kuahidi kuendelea kuishauri serikali ili kuendelea kuhifadi vizuri maeneo ya urithi.


Edward Ishengoma ni Kaimu kamishina wa wizara ya nishati amesema wao kama wahusika wakuu katika kusimamia mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambao unayekelezwa na serikali waliamua kuanzisha mradi huo ili uweze kuisadia nchi kwakuwa unafaida nyingi  tofauti la IUCN walivyokuwa wameishauri unesco .


“Mradi huu una manufaa makubwa sana tofauti na wao wanavyodhani kwa kuwa una manufaa kwanza  kimazingira ,kupata nishati , kuzuia mafuriko  na mengine mengi na hatutarudi nyuma “






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz