TAKUKURU yawafikisha wanne mahakamani uhujumu uchumi - EDUSPORTSTZ

Latest

TAKUKURU yawafikisha wanne mahakamani uhujumu uchumi



 
Mkuu wa Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo, amesema wamewafikisha mahakamani watuhumiwa wanne kati ya Aprili na Juni mwaka huu wakituhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi na makosa mengine mawili ya jinai.

Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani kwa makosa hayo ni pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Nangomba iliyopo wilayani Nanyumbu, anayetuhumiwa kughushi nyaraka za wafanyabiashara tofauti na kisha kuzishindanisha kuomba tenda ya kusambaza vifaa vya ujenzi, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mbali na watuhumiwa hao kufikishwa mahakamni katika kipindi hicho, pia taasisi hiyo imeeleza kuwa kesi 16 ziliendelea katika mahakama za Wilaya ya Mtwara, Masasi, Nanyumbu, Newala na Tandahimba na miongoni mwa kesi hizo mbili zilishatolewa uamuzi na Jamhuri, ilishinda.

Ngailo ametoa kauli hiyo leo mkoani Mtwara wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Takukuru kwa miezi ya Aprili hadi Juni mwaka huu.

Katika kipindi hicho Ngailo, amesema Takukuru ilipokea taarifa 89 za makosa ya rushwa na makosa mengine ya jinai na uchunguzi wake unaendelea.


 
Ametaja sekta zinazolalamikiwa zaidi katika taarifa hizo 89 walizopokea ni pamoja na Halmashauri yenye malalamiko 44,huku idara ya utawala ikiongoza kwa kuwa na malalamiko (18),idara ya ardhi (9),elimu, (6),Biashara(4),Ujenzi(3, huku utumishi na Tasaf kila moja ikiwa na malalamiko mawili

Ngailo, ametaja katika taarifa hiyo kuwa malalamiko mengine ni  kwa vyama vya ushirika yenye malalamiko(10), mifuko ya hifadhi ya Jamii(6),Mahakama(5),Polisi(4) maji(1),taasisi za dini(1) kodi lalamiko 1 na malalamiko binafsi yakiwa 25.

Aidha Ngailo, amesema katika kipindi hichowamefuatilia matumizi ya fedha za umma, katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,ambapo jumla ya miradi 15yenye thamani ya jumla ya zaidi ya sh. Bilioni 1.8 na baadhi zilikutwa na dosari ambazo walishauri namna ya kuziboresha.


Amesema katika kuelekea kipindi cha julai hadi septemba Takukuru mkoa wa Mtwara itajikita kutoa elimu kwa umma kwa lengo la kuwafanya wananchi kuchukua hatua na kushiriki mapambano dhidi ya rushwa na kuacha kuwa walalamikaji 

Wakati huo huo Ngailo, amesema wanafuatilia kwa kina taarifa za watu wanaogawa kwa upendeleo, pembejeo aina ya salfa,ambayo serikali inagwa bure kwa wakulima wa Korosho,mkoani humo.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz