Steve Nyerere Ampoza Manara "Shujaa hana thamani"


Msanii wa filamu Steve Nyerere ameshea comment yake kwa rafiki yake Haji Manara baada ya taarifa iliyotolewa na Klabu ya Simba kuhusu kuachana na aliyekuwa afisa habari wao Haji Manara kwa kusema hakuna jambo lisilokuwa na mwisho.


Kupiti ukurasa wake wa Instgram Steve Nyerere ameandika ujumbe mzito kwenda kwa Manara ambo unasomeka kama ifuatavyo.

"Rafiki inatosha kusema kila jambo lina mwanzo na mwisho, umefanya makubwa kwenye Simba, hakuna mashabiki wa Simba wasiojua ulicho kifanya, ulijitoa kwa moyo wako wote, sio rahisi sana watu wote kujua uliyokuwa unapitia lakini kama akijua Mungu na familia yako inakupasa kusema asante"

"Unakwenda kupumzika ukiwa umejenga uwezo mkubwa kwenye Mpira, wewe ni Binadamu lazima kwa nafasi uliyokuwa nayo maadui ni wengi kuliko watu wema, pokea na sema asante kwa kila jambo, uzuri wako hujawahi kubagua rafiki kwa kuchagua Yanga,Mtibwa, au Lipuli" 

"Tanguliza kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho na maliza kwa kusema shujaa hana thamani kwao, unabaki kwenye midomo ya watu, utaishi kwenye mifano mingi kwenye kila jambo la Simba, utakumbukwa na mkatokeo, Pumzika mdogo wangu, rafiki yangu kipenzi haina shida tuna kesho nyingi kuliko leo" ameongeza



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post