Shaffih Dauda "Simba Uzeni Miquissone na Chama Msiache Pesa Hizo" - EDUSPORTSTZ

Latest

Shaffih Dauda "Simba Uzeni Miquissone na Chama Msiache Pesa Hizo"Kuna tetesi kwamba, Simba imewekewa ofa na vilabu tofauti vikitaka kuwasajili Luis Miquissone na Clatous Chama.

Wachezaji ni asset ya klabu, kama inakuja ofa kama hizo ambazo zinatajwa [dola milioni moja], Simba wasilaze damu wanapaswa kuchukua huo mzigo kwa sababu wanaweza kupata wachezaji wengine wa daraja la juu na wakabaki na faida.

Miquissone ni mchezaji muhimu ndani ya Simba lakini kwa pesa hiyo, unaweza kupata wachezaji wa kiwango cha juu tena kutoka kwenye vilabu vikubwa vinavyoshiriki michuano ya CAF.

Kuhusu ofa ya Chama wala sijiulizi mara mbili, nachukua mzigo mapema kabisa. Chama ni kipenzi cha mashabiki, Ramos alikuwa kipenzi cha mashabiki pale Madrid lakini kaondoka!

Biashara ya mpira ukiweka mahaba mbele utabaki nyuma, Chama alipofika ni juu sana na aliyoifanyia Simba ni makubwa. Sioni kama anaweza kufanya makubwa zaidi ya hapo alipofika.

Ofa nzuri zikija ukazitupa, itafika wakati soko lake litashuka kwa hiyo muda huu wakati yupo kwenye kiwango cha juu na kuna vilabu vinamtaka ndio muda sahihi wa kufanya biashara. Waingize mzigo wakatafute Chama mwingine ambaye atakuja kufanya kazi kwa miaka minne ijayo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz