Shabiki wa Simba Afariki Dunia Kisa Yacouba wa Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Shabiki wa Simba Afariki Dunia Kisa Yacouba wa Yanga


Shabiki wa Simba, Kilosa Said (50+) wa Kijiji Cha mwamgongo (mwambao wa ziwa Tanganyika ) Mkoani, Kigoma amefariki Jana wakati akiangalia mpira wa Simba na yanga.

Rafiki wa Marehemu, Msafiri Ismail Shibu, amesema tukio hilo lilitokea walipokuwa wakiangalia mchezo huo wa Derby kwenye ‘Screen’ eneo la Mwamgongo.

“Tulikuwa tunaangalia mpira eneo la Mwamgongo, tulitandika turubai chini tukawa tunaangalia mpira kwenye `screen’ wakati Mchezaji wa Yanga, Yacouba Songné anafanya shambulizi kwenye lango la Simba presha ikapanda.

“Tukamchukua na kumpeleka hospitali, akawa ameshapoteza maisha, presha yake ilikuwa 250, Marehemu ameacha mke na watoto wawili,” Msafiri Ismail Shibu.

Kilosa anatarajia kuzikwa leo Julai, 26 saa 10, jioni katika kijini cha mwamgongo, mkoani Kigoma.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz