Mpangaji Afunguka A to Z Jinsi Alivyojaribu Kumsaidia Marehemu Zungu Akiungua na Moto Chumbani - EDUSPORTSTZ

Latest

Mpangaji Afunguka A to Z Jinsi Alivyojaribu Kumsaidia Marehemu Zungu Akiungua na Moto Chumbani


Majonzi yametawala Mbezi Makabe Dar es Salaam baada Msichana aiwate Grace Mushi maarufu kama Neema kudaiwa kumuua Boyfriend wake aitwae Hamis maarufu Zungu kwa kuichoma kwa petroli nyumba aliyokuwemo.

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni Mpangaji katika nyumba hiyo iliyochomwa moto.

"Nilikuwa nimelala nikashtuka mida ya saa 7 nilitaka kwenda chooni, nikaona mlangoni kuna uwazi kama unaingiza mwanga kwa ndani, nilivyofungua mlango nikaona moto umetanda karibia na chumba changu nikaanza kupiga kelele”


 TBS Internship Programme For Graduates - 54 Posts

“Nikauliza kuna nini mbona moto unawaka, ndio yule Kaka Zungu akaanza kusema Mama Su nipo naungua ndani huku moto umewaka nikamuuliza kuna nini Zungu akanambia Neema kanifungia mlango, nikamwambia fungua mlango akasema siwezi kufungua”

“Ilibidi nianze kufanya ustaarabu wa kumtoa mtoto wangu, nikwambia ngoja nitoke nje niombe msaada wa Watu kuja kunisaidia maana peke yangu siwezi akanijibu sawa Mama Su fanya haraka” 

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz