Mangungu Awataka Wanasimba Kuwa Watulivu Kuhusu Haji Manara na Barbara - EDUSPORTSTZ

Latest

Mangungu Awataka Wanasimba Kuwa Watulivu Kuhusu Haji Manara na BarbaraMwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amewataka wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuwa watulivu kuhusu yanayoendelea kati ya Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Msemaji Haji Manara na kuwahaidi kuwa baada ya mashindano, tathmini ya mwenendo mzima wa timu na watendaji wake itafanyika
Kauli hiyo imekuja baada ya msemaji wa klabu hiyo Haji Manara kumtuhumu Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kumfanyia chuki na kumtuhumu kuihujumu timu.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagramu Murtaza Mangunguameandika;

Wana Simba tuwe watulivu

Ninawaomba sana wanachama, wapenzi na washabiki wa Simba tuwe watulivu na makini kuelekea fainali ya FA CUP.

Uongozi wa Simba upo nakini na ulishatoa maelekezo ya kutatua mgogoro uliojitokeza.

Simba ni timu inayojipambanua kuendeshwa kiweledi, hivyo tusimame katika misingi hiyo.

Wote wanaolumbana ni waajiriwa na muajiri yupo.

Baada ya mashindano, tathmini ya mwenendo mzima wa timu na watendaji wake itafanyika.

Kwa sasa kila mmoja wetu azingatie nidhamu,hekima na misingi ya ajira au nafasi yake katika club.

Nawaomba tuwe watulivu na tuendelee na mikakati ya michezo ijayo.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz