Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamad Masauni, ametoa angalizo kwa baadhi ya Kampuni za simu kwa namna zinavyofanya promosheni yake kuhusu kodi ya serikali kwa njia ya miamala kwa kutoa taswira mbaya pekee na sio faida zitakazo mgusa mwananchi moja kwa moja.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na mabalozi hao walioteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba, kwa nyakati tofauti na kusema kwamba huduma ya makato ya miamala kutoka kampuni za mawasiliano imekuwa ikitozwa kwa anaetoa na anaepokea hivyo sio jambo geni.
Aidha Mhandisi Masauni ameongeza kuwa tayari Rais Samia alishatoa maelekezo kwa Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu kuunda timu ya wataalamu ili waweze kuona ni namna bora ya kuboresha kodi hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia marekebisho ya sheria.
Post a Comment