Maelfu Wamiminika Kumuona Ng'ombe Mbilikimo Zaidi Duniani - EDUSPORTSTZ

Latest

Maelfu Wamiminika Kumuona Ng'ombe Mbilikimo Zaidi Duniani
Watu wamekuwa wakifika kwa wingi katika shamba moja la mifugo huko Bangladesh kumuona kiumbe maarufu ng'ombe mbilikimo kwa jina Rani.

Ng'ombe huyo jike mwenye urefu wa sentimita 25 ana kilo 28 ana umri wa miezi 23.

Pamoja na amri ya kutotoka nje, zaidi ya watu 15,000 wameripotiwa kumtembelea Rani katika makazi yake huko Charigram, karibu na mji wa Dhaka.

Mkuu wa shamba hilo Hasan Howladar ameomba utambuzi wa Rani kwenye rekodi ya Guiness Book, akisema Rani ni ng'ombe mwenye umbo dogo zaidi duniani.


 
''Sijawahi kuona kitu kama hiki katika maisha yangu,'' mgeni Rina Begum ameiambia BBC idhaa ya Bangla.


Bwana Howladar alimnunua Rani mwaka jana katika shamba moja lililo kaskazini magharibi wilaya ya Naogaon.

Amesema ana changamoto ya kutembea na anawaogopa ng'ombe wengine walio katika shamba la Shikor Agro, hivyo amekuwa akimtenganisha na ng'ombe wengine.

''Hali sana.anakula kiasi kidogo cha majani mara mbili kwa siku,'' alisema Bw. Howladar. ''Anapenda kuzungukazunguka nje na anaonekana ana furaha tukimbeba.''

Rekodi ya ng'ombe mdogo zaidi ilikuwa ikishikiliwa na Manikyam, nchi jirani ya India, mwenye urefu wa sentimita 61.1 kutoka usawa wa kwato mpaka juu.


Bwana Howladar aliambia BBC kuwa wachunguzi kutoka Kitabu cha Guinness of Records watatembelea shamba lake mwaka huu ili kuona ikiwa Rani atachukua taji hilo.

Zikiwa zimesalia wiki chache tu kufika tamasha la Kiislam la Eid al-Adha, kumekuwa na uvumi juu ya ikiwa Rani atauzwa kwa ajili ya kafara. Lakini wakuu wa shamba walisema hawakuwa na mipango ya kuachana naye
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz