Kigoma Ina Wagonjwa 12 wa Corona



HABARI: Mkoa wa Kigoma umeripotiwa kuwa na wagonjwa 12 wa Corona ambapo wengine wamejitenga majumbani na wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika vituo vilivyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kulazwa wenye Corona.

 

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo mbele ya Kamati ya CCM, RC wa Kigoma, Thobias Andengeye amesema kanuni na taratibu za kiafya zinaendelea kufuatwa na kutoa tahadhari kwa wakazi wa Mkoa huo.

 

“Tuna wagonjwa 12 ambapo 6 wamelazwa na 6 wapo Majumbani wamejitenga na wanaendelea vizuri na matibabu,” amesema RC Andengeye.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post