Kesi Yake na Yanga, Morrison Aomba Mashabiki Wamuombee - EDUSPORTSTZ

Latest

Kesi Yake na Yanga, Morrison Aomba Mashabiki WamuombeeHayawi hayawi sasa yamekuwa, Jaji Patrick Stewart kutoka Uingereza hii leo ataisikiliza kesi ya Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans Sports Club dhidi ya mchezaji Bernard Morrison kabla ya kuitolea uamuzi.

 

Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick amesema hawezi kuzungumza chochote hadi kesi hiyo itakaposikilizwa. Morrison kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram amewataka wafuasi wake kumuombea na waliomtakia kila lakheri ni pamoja na CEO Barbara Gonzalez.

 

Ujumbe wa Bernard Morrison kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram; ”Even in the abundance of water , the fool will still be thirsty 🀦🏽‍♂️. Wish me well today πŸ’ͺπŸΎπŸ™ akimaanisha kuwa “hata kwenye maji mengi, mjinga huhisi kiu.”

 

Ikumbukwe kuwa, Kesi ya Yanga dhidi ya Morrison katika mahakama ya CAS inasikilizwa leo, hivyo wadau wa soka wapo macho kusikilizia nini kitaamriwa katika shauri hilo ambalo Yanga wanadai Morrison alisajiliwa SImba Sc wakati akiwa na makata halali na Yanga.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz