Kajala Achukua Uamuzi Mgumu Kwa Paula - EDUSPORTSTZ

Latest

Kajala Achukua Uamuzi Mgumu Kwa Paula 
KUFUATIA maneno mengi juu ya mwanawe, Paula Paul au Paula Kajala kutokwenda shule kwa maana ya kidato cha tano na sita, mama yake mzazi ambaye ni staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja amechukua uamuzi mgumu kwa mwanawe huyo.
Kajala ameliambia gazeti hili la IJUMAA kuwa, ni lazima ampeleke mwanawe huyo shule kwani yeye ndiye mwenye jukumu la kumsomesha.Hata hivyo, kabla ya kumpelea Paula kidato cha tano na sita, sasa amebadili uamuzi wa awali wa kumsomesha kwenye shule za ndani ya Bongo, badala yake ameamua kumtafuta chuo nje ya nchi ambako atakuwa na utulivu zaidi kwa sababu amechoka kusema mno.

Kwa sasa Paula amekuwa gumzo na wengi kutoamini kama anaweza tena kutulia darasani na kusoma baada ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny au Chui.

Miongoni mwa mambo yanayotrendi tangu jana ni pamoja na picha za wawili hao wakioneshana mahaba laivu baada ya kujifichaficha kwa muda mrefu, lakini sasa ni mwendo wa kujiachia tu.

Hata hivyo, mmoja wa wafuasi wa Paula kwenye ukurasa wake wa Instagram alimuuliza mrembo huyo kwamba amechaguliwa kujiunga na shule gani ambapo alimjibu; “Next Level Music…” Ambayo inafahamika kwamba ni lebo ya muziki inayomilikiwa na Rayvanny.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz