Julius Malema Afungiwa Kutumia Twitter kwa Muda

 


Kiongozi wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) nchini Afrika Kusini bwana Julius Malema amezuiwa kwa muda kuandika katika kwenye akaunti yake ya tweeter kwa kukiuka miongozo ya Twitter , vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Mbuyiseni Ndlozi, mbunge na mwanachama wa chama cha EFF, Jumanne aliweka picha ya ujumbe ambao unaonesha kuwa bwana Malema amezuiwa kwa muda kuandika kwenye twitter.


Bwana Malema amezuiliwa kuandika na kushiriki ujumbe wa wengine kwenye akaunti yake ya twitter kwa muda wa takribani saa 12.


Bwana Malema alitishia kuhamasisha wafuasi wake kushiriki katika vurugu kubwa ambazo zinapinga kufungwa kwa Zuma, zilizoanzia KwaZulu-Natal na jimbo la Gauteng .


“Hatutaki askari mtaani kwetu ! La sivyo, tunaungana na wanaoandamana.Wapiganaji wote wote wanapaswa kuwa tayari...hawawezi kutuua sisi sote. Tunataka suluhu ya kisiasa katika tatizo la kisiasa na sio wanajeshi ,” bwana Malema aliandika kwenye Tweeter akipinga wanajeshi kukabiliana na maandamano.


Rais Cyril Ramaphosa alitoa agizo kwa wanajeshi kwenda katika majimbo mawili kusaidia kuzuia ghasia zilizosababishwa na kufungwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma.


Bwana Ramaphosa alitoa onyo kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya wanaoweka maudhui au taarifa za uongo na uchochezi mtandaoni.


Mamlaka imesema watu wapatao 12 wanachunguzwa kwa kuhamasisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii.


Waziri wa kushughulia masuala ya polisi Beki Cele alisema wanafanyia uchunguzi ujumbe wa Twitter na binti wa Zuma, Dudu Zuma-Sambudla, kukosoa utendaji wa sheria.


Akaunti ya Dudu ilishirikishwa mtandaoni ilikuwa inaikosoa serikali na kusifia au kuwahamasisha waandamanaji wanaopinga kufungwa kwa baba yake.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post