Hoteli yaporomoka China, Watu Wanane Wamepoteza Maisha - EDUSPORTSTZ

Latest

Hoteli yaporomoka China, Watu Wanane Wamepoteza Maisha

Watu wanane wameuawa wakati jengo la hoteli lilipoporomoka huko Suzhou, mkoa wa Jiangsu nchini China.

Jitihada za uokoaji zinaendelea kwa wale waliokwama chini ya kifusi.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Usimamizi wa Dharura, ilitaarifiwa kuwa timu za utaftaji na uokoaji zilitumwa kwa mkoa huo na maiti za watu 8 zimepatikana hadi sasa.

Katika taarifa hiyo, imebainika kuwa watu 14 waliokolewa kutoka kwenye kifusi cha hoteli na watu 9 hawakupatikana.

Imeelezwa kuwa hoteli hiyo iliyo na vyumba 54 ilifunguliwa 2018.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz