Haji Manara "Vitimbi Mnavyonifanyia Kisa Simba Vimenichosh" - EDUSPORTSTZ

Latest

Haji Manara "Vitimbi Mnavyonifanyia Kisa Simba Vimenichosh"Maneno ya Hajismanara yaliyoacha mafumbo kwa mashabiki na wapenzi wa soka.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika haya.

"Hivi vitimbi mnavyonifanyia kila siku kisa Simba vishanichosha ,,,mwisho wa siku mtanitoa roho yangu kabla ya muda wangu...
Imetosha kwa sasa !!

Ubaya wote ni Haji lakini mafanikio ni yenu nyie Wakubwa..
Kila siku ni Haji Haji Haji..

Mkitoka kunisingizia hili mtatengeneza cinema nyingine kwangu,,tunashindwa kujua kila Mja Mungu kampa fungu lake,,,,inakuwaje Rizki ya umaarufu wa mwenzio iwahangaishe kiasi hcho?
Likinitokea baya pakuanzia mnapo.

Asanteni ndugu zangu na Mlipaji ni Mungu na ukweli utajulikana

IMETOSHA" HAJIS MANARA

"Unaniuliza na kujaribu kulaumu kwa nn iwe leo tukijiandaa na game ngumu?

Ndugu zangu wapendwa hakuna hata mmoja kati ya tunaosema hivyo anaeweza kuvumilia nusu ya hayo niliyofanyiwa.

Kifua changu kipana mno na kimebeba machungu mengi yaliyokaribia kuutoa uhai wangu!!

Ila nawasihi tulieni tumalize mechi na tuombe uhai.

Wengi wanadhani nimekurupuka,,laa hasha Guys..

Tuwe na subira na tuombe salama kigoma.

Baada ya kauli hii nimemaliza, sisemi kitu hadi game ipite, nilikuwa nisiseme lakini nimeshauriwa niwaambie ukweli Wanasimba na Watanzania.

InshaAllah iwe Kheri kwetu huko. 🙏" HAJIS MANARA


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz