Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Sunday Manara, amewashukia baadhi ya Mashabiki na Wanachama wanaosaka visingizio, baada ya timu yao kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans jana Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wamekua wakimlalamikia Mwamuzi Emmenuel Mwandembwa kwa kuwepa video fupi kwenye mitandao ya kijamii, inayoonesha beki wa Young Africans Dickson Job akizuia mpira kwa mkono uliopigwa na Morisson, huku wakudai ilikua penati halali, ambayo haikukubaliwa na Mwamuzi huyo kutoa Arusha.
Kitendo cha baadhi ya Mashabiki na Wanachama hao kulalamika kimemkera Manara na kuandika ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Manara ameandika: Mm sipendi Baadhi yetu tunavyoifanya hii ni Agenda ya sisi kukosa matokeo jana..
Sometimes waamuzi nao ni binadaam sio Robot.
Tuangalie wapi tulipojikwaa no matter tunachosema tulikosa bahati.
Hatupaswi Kwa ukubwa wetu kuzungumzia pungufu hili,,tulipaswa kushinda tu au kukubali dhana ya Game of Chance.
Shida ya wengi ni kutokuwa wavumilivu na utani wa mtaani au mitandaoni,,,Yashakuwa na hayabadiliki matokeo ya jana,,,Muhimu ni kutulia kisha tutarajie benchi na wachezaji wetu kuja Kwa nguvu ktk fainali ya Kigoma.
Huo ndio ukatili wa football na maajabu yake.... yatupasa kujiuliza na kutetea taji letu kisha come back yetu ifanane na Simba Sports Club.
No comments:
Post a Comment