Waziri akataza adhana isitolewa kwa sauti kubwa, Sheikh amtaka aombe radhi wenzake wamgeuka - EDUSPORTSTZ

Latest

Waziri akataza adhana isitolewa kwa sauti kubwa, Sheikh amtaka aombe radhi wenzake wamgeuka




Viongozi wa Kiislamu nchi Muslim Burundi wamejitenga na kauli iliyotolewa na mmoja wao kumkosoa waziri wa mambo ya ndani aliyetoa wito kwa mashekhe kupunguza sauti ya adhana ya asubuhi ili isiwe kero kwa umma.



Katika kikao cha pamoja na viongozi wa kidini, Waziri wa Mambo ya ndani wa Burundi Gervais Ndirakobuca aliwaomba viongozi kidini wasipige kelele wakati wa maombi ya usiku na kwa wenzao wa Kiislamu kupunguza sauti ya Adhana (wito wa sala) wakati wa alfajiri.

Jumanne asubuhi Ndikumana Rashid, alisikika akimkaripia waziri na kumtaka afutilie mbali matamshi aliyotoa na kuomba msamaha.

Bw. Rashid alisema kauli ya waziri ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya dini ya Kiislamu.

Wawakilishi wa Waislamu hata hivyo wamesema Bw. Rashid atawajibikia kauli yake kwa kumtukana waziri.

Kwa mujibu wa BBC. Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Burundi Zuberi Mohamed, amesema hakuna mzozo kati ya Waislamu na serikali akiongeza kuwa wito wa sala jimbo la kawaida.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz