Rais Samia: Mazungumzo ya Bandari Bagamoyo Yanaendelea - EDUSPORTSTZ

Latest

Rais Samia: Mazungumzo ya Bandari Bagamoyo Yanaendelea





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa bandari ya Bagamoyo pamoja na kufufua mradi wa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma kwa kuwa soko la chuma kwa Dunia limepanda.

 

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 26, 2021, mkoani Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.

“Kuhusu bandari ya Bagamoyo tumeanza mazungumzo ya kufufua mradi wote ule wa Bagamoyo pamoja na Mchuchuma na Liganga nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika zinaendelea na mazungumzo kuona tatizo ni nini” amesema Rais Samia

 

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa“Kuhusu Mchuchuma na Liganga mazungumza yanaendelea kuona tatizo ni nini serikali inaweza kujitoa mpaka wapi, mwekezaji ajitoe mpaka wapi na taarifa zilizopo Duniani chuma imepanda bei ni wakati mzuri wa kuharakisha na kufanya ule mradi”






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz