Muuwaji wa George Floyd kujua adhabu yake leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Muuwaji wa George Floyd kujua adhabu yake leo
Mahakama ya mji wa Minneapolis nchini Marekani inatarajiwa leo kutaja adhabu atakayopewa Derek Chauvin, polisi mzungu aliyekutwa na hatia ya kumuuwa Mmarekani mweusi George Floyd. 
Mwezi Aprili jopo la majaji maalumu lilimkuta Chauvin na hatia ya mauaji yasiyo ya kupanga, nchini Marekani yakijulikana kama mauaji ya daraja la pili. 

Upande wa uendeshaji mashtaka unataka Chauvin apewe kifungo cha miaka 30 jela, huku upande wa utetezi ukitaka adhabu atakayopewa aitumikie bila ulazima wa kupelekwa gerezani. 

Kifo cha kusikitisha cha Floyd kilichotokea tarehe 25 Mei 2020 kilisababisha maandamano kote duniani, ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukalitili wa polisi nchini Marekani. 

Kifo hicho kilirikodiwa katika mkanda wa vidio, uliomwonyesha afisa Derek Chauvin akimgandamizia goti shingoni akiwa amelala sakafuni kwa karibu dakika tisa, huku akilalamika kuwa hawezi kupumua. 

Polisi walikuwa wamemkamata Floyd kwa tuhuma za kutumia noti bandia ya dola 20.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz