Mtoto wa Monalisa alamba dili nono la ubalozi





 Binti wa Staa wa filamu nchini Monalisa ameingia mkataba wa kuwa Balozi wa taulo za kike za Lavy  za mwanamitindo Flaviana Matata.
Soania ambaye mwaka huu amehitimu kidato cha sita Shule ya Sekondari Tusiime alikochukua masomo ya biashara (ECA) ame-share habari hiyo njema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Monalisa amempongeza binti yake kwa hatua hiyo kubwa sambamba na kumshukuru Mungu. "Mungu wetu ni mwema kila wakati. Hongera sana binti yangu @soniamonalisa" - ameandika @monalisatz kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kadhalika na hilo @soniamonalisa ni msanii wa muziki na tayari ametoa ngoma mbalimbali ikiwemo ‘Mama Yake Sofia’ na ‘Bye’ aliouachia mwezi uliopita.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post