Mrembo wa Mondi amtisha Zari - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mrembo wa Mondi amtisha Zari
UBUYU wa ndani kabisa unadai kwamba, baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ alifikia hatua ya kusitisha uwepo wake Bongo, muda mfupi baada ya kusambaa kwa tetesi za jamaa huyo kudaiwa kuwa na mrembo mpya, IJUMAA limepenyezewa.

 

Katika hali ya kuonekana kama kuwaaga Wabongo, mwanamama huyo aliwashukuru pia wakosoaji wake akidai kwamba waendelee kumkosoa kwani kwa kufanya hivyo wanamjenga zaidi.

 

Itakumbukwa kwamba, wiki iliyopita, Zari alitua Bongo kwa ajili ya kugawa taulo za kike na kutinga bungeni kama Balozi wa Hiyari wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

 

Katika safari yake hiyo aliambatana na wanawe wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan aliozaa na Diamond au Mondi kwa ajili ya kumsalimia baba yao.

Katika maelezo yake wakati anatimka Bongo, Jumapili iliyopita, Zari alisema ilikuwa ni safari nzuri kwake.Hata hivyo, kuondoka kwa Zari aliyefikia nyumbani kwa Mondi pale Mbezi-Beach jijini Dar kulikuwa kwa ghafla mno na haikutegemewa kwani ilifahamika kwamba angekaa Bongo kwa muda mrefu.

 

Hii ni kwa sababu katika moja ya intavyu mara tu baada ya kutua Bongo, Zari alisema angekaa Tanzania kwa zaidi ya siku saba hivyo kuondoka kwake kuliibua viulizo vingi.Hata hivyo, habari za ndani zinadai kwamba, kuondoka ghafla kwa Zari kulikuja muda mfupi baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa, Mondi au Simba amenasa kifaa kipya ambacho ni mwanamitindo maarufu wa nchini Afrika Kusini (Sauzi).

 

Gazeti la IJUMAA limenasa jina la mrembo huyo ambalo ni Andrea Abrahams.Tetesi za Mondi kunasa kwenye penzi la mrembo huyo zililipuka mara baada ya Andrea kuonekana akiwa amezaa koti kubwa la Mondi alilokuwa amevaa wakati alipoweka kambi nchini Afrika Kusini hivi karibuni kwa ajili ya kuandaa albam yake mpya itakayotoka baadaye mwaka huu.

 

Wawili hao; Mondi na Andrea ni marafiki kupitia mtandao wa Instagram kwani kila mmoja amem-follow mwenzake. Tetesi hizo zimezidi kushika kasi kufuatia mrembo huyo kuapa kumfuata Mondi popote atakapokuwa.

 

“Nitakuwa nyuma yako muda wote,” ameandika mrembo huyo katika moja ya picha za Mondi.Katika moja ya video ambazo Gazeti la IJUMAA limeziona, Mondi na Andrea wanaonekana wakizungumza na kuchati kupitia Insta Live.Katika video hiyo, Andrea anasikika akimwambia Mondi kuna mtu alimuuliza ni wapi alipokutana naye.“Kuna mtu ameniuliza leo mimi na wewe tulikutanaje?” Anasikika Andrea akimwambia Mondi.Katika majibu yake, Mondi anaonekana na kusikika akisema; “Sijui…” kisha akaondoka hewani huku akimmwagia mabusu kama yote.

 

Mrembo Andrea anaibuka kwenye maisha ya Mondi ikiwa ni miezi kadhaa tangu ilipoaminika kuwa anamiliki kifaa kutoka Ethiopia.

Miezi kadhaa iliyopita, Mondi alinaswa na mrembo huyo wa Ethiopia huku kukiwa na madai mazito kwamba huwenda ndiye angeolewa na staa huyo anayewania Tuzo ya BET.

 

Andrea anatajwa kuwa na sifa za kimaumbile na rangi ambazo Mondi huwa anapendelea akifananishwa na Tanasha Donna hivyo kuna uwezekano mkubwa akaolewa na jamaa huyo ambaye ametangaza kuoa mwakani.

 

Hadi sasa, Mondi ana kijiji cha wanawake aliotoka nao huku akizaa na watatu ambao ni Zari, Hamisa Mobeto na Tanasha.

Stori: Mwandishi Wetu, DAR
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz