Mobeto Amkimbiza Mchumba wa Rick Ross - EDUSPORTSTZ

Latest

Mobeto Amkimbiza Mchumba wa Rick Ross




STORI kubwa kwenye mitandao ya kijamii imeendelea kumhusu mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto kwamba, yupo kwenye mawasiliano ya kimapenzi na megastaa wa Hip Hop wa Marekani, William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’.

 

Sasa, ubuyu huo umezaa mazito kwa sababu unadaiwa kumkimbiza mchumba wa Rick Ross au The Boss aitwaye Tommie Lee; bonge moja la mrembo wa haja pamoja na kwamba ni mama wa watoto wawili.


Megastaa wa Hip Hop wa Marekani, William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’.

 

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za udaku wa mastaa wa Marekani uitwao @theshaderoom, Tommie Lee; baada ya kuona ukaribu wa Rick Ross na Mobeto na jinsi wanavyochati kila kukicha, ameamua kubwaga manyanga.

 

“Tommie; ifahamike kwamba yeye (Tommie) na Rick Ross ni marafiki tu na patna wa kibiashara na si vinginevyo,” umeandika mtandao huo wa kuaminika huku ukipambwa na picha kubwa ya Mobeto



Mara ya mwisho kwa Tommie Lee kuonekana hadharani akiwa na Rick Ross ilikuwa ni katikati ya mwezi Mei, mwaka huu ambapo wawili hao walinaswa kwenye klabu moja usiku huko Miami nchini Marekani.

 

Tangu kusambaa kwa habari za Mobeto na Rick Ross, Tommie Lee ambaye ni mwanamitindo na rapa hajaonekana tena na jamaa huyo.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Tommie Lee amefunguka; “Nipo singo kwa hiyo mwanamke yeyote anayekuja kwenye ukurasa wangu kunishambulia, anishambulie mimi na siyo mtu mwingine.“Samahani (Rick) Ross ni rafiki na mbia wa kibiashara na hakuna kingine.



”Kwa mara ya kwanza, Rick Ross au Rick Rozay ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Maybach Music Group, alianza kuchati na Mobeto baada ya mwanamama huyo kufanya intavyu kubwa na bosi wa kinywaji maarufu duniani aitwaye Brett Berish.

 

Itakumbukwa kwamba, Rick Ross ni balozi mkubwa wa kinywaji hicho na sasa amemuunganisha Mobeto naye kuchukua ubalozi huo.

 

Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA hivi karibuni, Mobeto alikiri kwamba Rick Ross ni kati ya mastaa wakubwa wa muziki anaowakubali na kutamani siku moja afanye naye kazi.

STORI; SIFAEL PAUL
M




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz