Mashoga waliojaliwa pacha watatu wasimulia safari yao ya mapenzi - EDUSPORTSTZ

Latest

Mashoga waliojaliwa pacha watatu wasimulia safari yao ya mapenzi

Wanandoa Mashoga Waliojaliwa Pacha Watatu Wasimulia Safari yao ya Uzazi
Jake na Sean walijaliwa watato hao mnamo Februari na wanashirikina kuwalea malaika hao.Picha:Daddies three.
Wakizungumza na CBS News, Jake na Sean wameelezea safari yao ya kuwa baba kama tukio lililobadilisha maisha yao.

Sean alisema anawapenda sana watoto wao na upend huo umekiwa ukiongezea tangu kuwasili kwao.

"Moyo wako unakua karibia mara kumi. Nahisi kwamba ni upendo mwingine tofauti ambao nimewahi kukumbana nao.Nitakuwa kwa ajili yao,” Sean alisema.


 
Jake alisema kwa upande wake alisema mapenzi yake kwa Sean yaliongezeka zaidi baada ya kushuhudia namna anawajibikia vyema wajibu wake kama baba.

"Ilinifanya kumpenda Sean zaidi. Kukmuon atu kama baba na hata kuwajibika japo najua amechoka sana. Tumewalea pacha hao kama timu," alisema.

Jake na Sean walitumia njia ya uzazi wa wakala kupata watoto hao na kuchapisha safari yao kwenye Tik Tok.


Walikulia katika dini ya wokovu

Wanandoa hao ambao walikutana mwaka 2012 walikulia katika dini ya Mormon ambapo walifunzwa ushoga ni dhambi.

Kulingana na wawili hao, walijaribu kusaidiana kuepuka kuwa mashoga na kuoa wake wema lakini waliishia kupendana.

"Sisi ni wapenzi. Tulianza kama vijana wa Mormon kujaribu kuchambua maisha. Tulikuwa marafiki wa karibu kisha tulipendana," alisema Jake.

Kutokana na kuwa waumini wa dini ya Mormon, wawili hao hawakutambua endapo familia zao zitaunga mkono uamuzi wao.


 
"Wazazi wangu walishuhudia nikipitia wakati mgumu wa kutaka kujitoa uhai. Na kwa sababu walitaka kuniona nimefurahi walikubali,” Sean alisema.


Kisha baadaye walioana mwaka 2016 baada ya wazazi wao kuwakubalia.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz