Hatimaye Aunt Ezekiel na Jack Wolper Wamaliza Bifu - EDUSPORTSTZ

Latest

Hatimaye Aunt Ezekiel na Jack Wolper Wamaliza Bifu

 


LILE bifu lililokuwa bab’kubwa kati ya waigizaji Aunt Ezekiel na Jacqueline Wolper, limezikwa rasmi na sasa wawili hao wanaishi vizuri.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, wawili hao walipatanishwa kwenye hafla ya Komunio ya mtoto ya muigizaji mwenzao Irene Uwoya (Krish Ndikumana) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hekima Garden, Mikocheni jijini Dar wikiendi iliyopita

Chanzo kimoja makini kilisema siku hiyo, Wolper alifika kwenye meza aliyokuwa amekaa Diamond na timu yake na ndipo Juma Lokole alipomvuta na kumtaka wakumbatiane na Aunt.

“Walipatanishwa na Juma Lokole na kuanzia hapo wamekuwa marafiki upya na hakuna tena anayeweza kuwa na kinyongo. Kifupi wamesameheana,” kilizungumza chanzo makini.

RISASI limefuatilia mawasiliano ya wawili hao kwa sasa na kubaini yamerudi kama zamani na kwamba hawakutaka kujua mchawi ni nani zaidi ya kuzika tofauti zao.“Wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite

Hakuna kukumbushana madeni wala nini na bahati nzuri sasa hivi Wolper ana furaha isiyo kifani ya kupata mtoto basi mambo yamekuwa safi kabisa,” kilisema chanzo makini.

Wawili hao waliingia kwenye bifu zito kufuatia Wolper kudai kumkopesha nguo Aunt na kisha mwenzake huyo kukataa kulipa kwa kipindi kirefu.

STORI NA MWANDISHI WETU, RISASI

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz