DC Mpya wa Kisarawe Atoa Neno - EDUSPORTSTZ

Latest

DC Mpya wa Kisarawe Atoa Neno

 


MKUU wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amefunguka baada ya kuapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kuwa Mkuu wa wilaya hiyo.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa  Instagram Nikki wa Pili ameandika kuwa “Kwanza namshukuru Mungu, pili Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Kisarawe na Serikal

“Nina ahidi kutumia vipawa vyangu, busara zangu na uwezo wangu kuifanya kazi hii nikishirikiana na watumishi wenzangu pamoja na wananchi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Shukrani kwa wote walio nitumia salamu za pongezi na mimi nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano” Zaburi 121:5 ameongeza





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz