Maneno Mabaya 10 ya Kutosema Kwa Mwenza Wako - EDUSPORTSTZ

Latest

Maneno Mabaya 10 ya Kutosema Kwa Mwenza Wako


 Mojawapo ya nguzo kuu kabisa ya mahusiano mazuri ni mawasiliano. Mawasiliano mazuri yanahusisha vitu viwili vikubwa, kuwa na ujumbe wa kusema na namna ya kusema ujumbe wako.

Maneno ni kitu hatari sana katika mahusiano yakitumiwa vibaya na yakitumika vizuri ni nguzo kubwa ya mahusiano mazuri na yenye furaha.

Hivyo unatakiwa kupangilia maneno yako unapoongea na mwenza wako ili kupata athari chanya. Ifahamike kuwa maneno mabaya yakisha semwa hayarudi mdomoni na madhara yake yatabaki siku zote hata kama mwenza wako atasema kuwa amesamehe au kusahau.

Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.

Maneno 10 Mabaya Ambayo Hutakiwi Kusema Kwa Mwenza Wako:

  1. Maneno ya Matusi

Maneno kama “mjinga” au “mpumbavu” yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.

Useseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama “sura mbaya”,”Mnene kama nguruwe” n.k

  1. “Nakuchukia”

Chuki ni kitu kikubwa sana,kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa “Nachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani” au maneno yanayofanana na hayo.

  1. “Ameiga Tabia Zako”

Wazazi wanatabia ya kurusha lawama kwa wenza wao pale watoto wanapokuwa na tabia mbaya. Utasikia mzazi mmoja akisema kwa mtoto “Tabia za mama yako hizi” au “Tabia za baba yako” pale mtoto anapoonesha tabia mbaya. Maneno haya hayafai kutumika katika familia kwakuwa yanashambulia nafsi ya mwenza wako.

  1. Kumfananisha Tabia Mbaya za Mwenza na Wazazi Wake

“Tabia zako kama mama yako”, au “..kama baba yako” maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.

  1. “Acha!Nitafanya Mwenyewe”

Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu,maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.

  1. Maneno Mabaya ya Kukatisha Tamaa

“Hutaweza” ,”Hutafanikiwa” n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo.Soma:  Namna ya Kukabiliana na Tabia ya Kuhukumu Watu Wengine

Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.

  1. “Mtoto wangu”

Itambulike kuwa hakuna mtoto wa mtu mmoja,wenza wote wawili wana haki na wajibu sawa juu ya mtoto wao. Najua mila na desturi zimetufundisha tofauti juu ya haki juu ya mtoto kwa wazazi wawili lakini ukweli ni kuwa wazazi wote wana nafasi na haki sawa kwa mtoto wao.

  1. “Haya yote ni makosa yako”

Lawama hazijengi bali zinabomoa. Lawama zinavunja moyo kwa mwenza wako. Pale panapotokea shida au matatizo kati yenu ni vyema kuyachukua kama yenu wote na mtafute suluhisho kwa pamoja.

  1. Kutolea Mifano Mahusiano ya Zamani

Usithubuthu kumfananisha mwenza wako na mpenzi wa zamani hata kama wazamani alikuwa bora zaidi kwa vigezo vyako. Mfano “John alikuwa ananitoa sana,lakini wewe hufanyi hivyo” au “John alikuwa anapenda sana chakula hiki”

  1. Maneno juu ya Kuachana

Usitumia maneno yanayoashiria nia ya kuachana,yanaondoa imani juu ya masiha ya mahusiano yenu.

Mfano “Kwa mtindo huu mimi nafikiri hatutafika mbali”

Mwenza wako ataanza kujiandaa kuachana na hatajiachia kwa asilimia zote kwa mapenzi na mipango ya pamoja. Maneno haya yanajenga utengano taratibu ndani ya moyo wako na wa mwenza wako.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz