KUNA NYAKATI NGUMU KATIKA MAPENZI, Zijue Hatua za Kuchukua! - EDUSPORTSTZ

Latest

KUNA NYAKATI NGUMU KATIKA MAPENZI, Zijue Hatua za Kuchukua!


Pata GB 20 Mitandao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 NI Jumapili tulivu kabisa, kwa uwezo wake Mola tunakutana kwenye kilinge chetu hiki cha malovee, mahali pekee pa kujifunza kuhusu maisha ya uhusiano.

 

Hapana shaka hapa tunajifunza mambo mbalimbali yanayotusaidia kustawisha uhusiano wetu, karibu upate somo jipya.

Kama mada inavyojieleza hapo juu, kwenye uhusiano wowote hususan wa mapenzi, zipo nyakati ngumu.

 

Kwa kawaida, kila anayeingia kwenye uhusiano huwa anatarajia kuishi vizuri.

Hakuna anayetaka kuishi kwenye matatizo au shida mbalimbali, lakini hizi hutokea kama vile ajali, upende au usipende unaweza kujikuta kwenye nyakati ngumu.

 

Nyakati ngumu huwa zinahitaji moyo wa ziada kuzipita, ukiwa na roho nyepesi unaweza kukata tamaa. Unaweza kushindwa kuvuka.

Nyakati ngumu zaweza kuwa za matatizo kati yenu, zaweza kuwa mtihani wa kukosa kazi, zaweza kuwa misiba, ugonjwa na matatizo mengine ya dunia.

 

Hivi ni vipindi ambavyo ili mvuke, lazima muamini kwamba maisha si raha tu, kuna karaha na maudhi. Kuna maradhi na matatizo mengi tu ambayo hatuwezi kuyamaliza tukiyaorodhesha hapa.

 

Lakini msingi wa hoja yangu ni nini? Nataka sote tuzifahamu hizi nyakati ngumu na tuwe na moyo mpana wa kukabiliana nazo.

Unapokuwa na mwenzako kwenye uhusiano, jua kwamba umebeba dhamana ya kufa na kuzikana.

 

Unaweza wewe kupata mtihani au yeye. Hivyo dhamana hii ni yenu wote wawili, kila mmoja wenu atambue kwamba ana dhamana ya kumjali mwenzake.

Roho ya uhusiano wenu mnaishikilia ninyi wawili. Mnao wajibu wa kufurahi pamoja na kusikitika pamoja pale mnapokuwa kwenye wakati mgumu.

 

Ndugu zangu, nyakati ngumu ni sehemu ya maisha. Chunga sana usije kimbia au kuepuka pindi mnapokuwa kwenye nyakati ngumu.

Ukomavu au kipimo cha utu siku zote huwa ni kwenye nyakati ngumu. Mnapovuka salama kwenye kipindi hicho, si tu kwamba mnastahili pongezi, lakini mnadhihirisha kwamba ninyi mnastahili tuzo ya ubinadamu.

 

Mathalan mwenzako amepata ajali, amepoteza baadhi ya viungo au ameugua muda mrefu, hizi ndizo nyakati ngumu, pambana!

Imetokea mpo kwenye malumbano yasiyokwisha labda pengine kwa mmoja wenu kufanya kosa kubwa, hizo ni nyakati ngumu, usikate tamaa.

 

Wewe ni sehemu ya suluhisho, tambua kama maisha si kutangatanga, pigania penzi lako kwa gharama yoyote.

Ndugu zangu, wengi tunaowaona wamefika mbali kwenye ndoa au uhusiano wao, wamekwepa mishale mingi.

 

Wamepitia nyakati ngumu sana ambazo wakikuhadithia unaweza usiamini, lakini ndiyo ukweli.

Ili na wewe uwe sehemu ya mafanikio, lazima ukubali kujitoa, kupambana kwenye nyakati ngumu hadi ufanikiwe.

 

Usiwe na moyo mwepesi wa kukata tamaa, tambua kwamba maisha yana raha na matatizo. Kuna milima na mabonde.

Inapotokea mmeingia kwenye nyakati ngumu, usiwe mtu wa haraka sana kufanya uamuzi. Vuta subira ili uione hekima inataka nini katika jambo husika.

 

Wengi sana wamefanikiwa kwenye migogoro ya uhusiano kwa kujipa nafasi, kutokurupuka kufanya uamuzi. Jipe muda wa kutafakari kabla ya kufanya jambo lolote lile.

Amini uliyenaye ni wako. Huna sababu ya kukimbia kihunzi chochote kile kitakachokuja mbele yenu. Iwe ni ugonjwa au ugomvi komaa utoke salama.

 

Marafiki, nyakati hizi siri kubwa ya ushindi ni kumuamini Mungu. Kumuomba awavushe salama.

Mikiamini kwake hakuna litakalowashinda. Mtangulizeni Mungu, hakika mtafanikiwa hadi ninyi wenyewe mtashangaa mmevukaje.

 

Muhimu ni kujua safari yenu mliyoianza maishani ni muhimu kuliko jambo lolote, mkiamini kila linalokuja mbele yenu ni sehemu ya maisha, basi mtaishi sana.

Ni matumaini yangu mtakuwa mmenielewa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.


Pata GB 20 Mitandao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz