NAMNA YA KUISHI NA MWANAUME MWENYE WIVU WA KUPINDUKIA! - EDUSPORTSTZ

Latest

NAMNA YA KUISHI NA MWANAUME MWENYE WIVU WA KUPINDUKIA!

Pata GB 20 Mitandao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Wivu ni moja kati ya ishara za mapenzi, katika mapenzi kama mwenza wako haonyeshi hata kawivu kidogo hainogi na hata kama anakupenda wakati mwingine unaweza kujihisi kama hakupendi. Lakini kama ukizidi basi wivu ni risasi ya kuua mapenzi. Inakera sana kuwa na mwenza ambaye ana wivu wa kupindukia, ambaye anauliza kila kitu unachofanya, anakufuatilia kila sehemu, hataki uongee na watu wengine hasa wa jinsia tofauti anakukataza kufanya baadhi ya mambo na vitu vingine kama hivyo.

Kwa mwanamke ni mbaya zaidi kwani mwanaume mwenye wivu ni kama kichaa anaweza hata kukukataza kufanya kazi au hata kama akikuruhusu kufanya kazi au biashara akakuharibia katika kazi yako na hata biashara yako. Ni vigumu kwa mtu mwenye mpenzi wa namna hii kuwa na furaha katika maisha yake kwani ni kama kamdudu kanakusumbuasumbua kwenye nguo, kanaweza kakawa hakakung’ati lakini ile kupitapita kwenye nguo ikatosha kukufanya utamani hata kufa!

Mwanaume mwenye wivu atakua na wasiwasi katika kila kitu, atakua anafuatilia simu yako, atakua anagombana na kila rafiki yako na kila mwanaume unayeongea naye akili zake zitamtuma kama ni mpenzi wako. Inakera sana kwani wengine hufikia hatua ya kukukataza kufanya kazi, kuwa na marafiki hata wanawake, kukukataza kuhudhuria misiba na sherehe na hata kukataza kuwasiliana na ndugu zako. Kama unaishi na mwanaume wa namna hii, awe ni mpenzi wa kawaida au mume basi mbinu zifuatazo zitakusaidia kuishi kwa furaha.

(1) Ongea Na Mwenza Wako Kuhusu Kile Kinachompa Wivu, Uoga Wake; Kua na wivu inamaanisha kuna kitu ambacho kinamsumbua, kitu ambacho anahisi utakifanya. Hembu anza kwa kuongea naye, tafuta muda ambao ametulia na muambie namna ambavyo wivu wake unakusumbua, namna ambavyo huna furaha kwasababu ya yeye kukufuatilia. Mhakikishie kuwa unampenda na muambie akuambie ni kitu gani hasa ambacho umeshawahi kukifanya mpaka kumfanya kuwa vile.

Muache aongee, atajaribu kutukana na hata kukuita Malaya, atatunga mambo mengi ambayo wewe hujayafanya lakini usipaniki na kuanza kujitetea. Hapana msikilize mpaka mwisho na akishamaliza wewe pia ongea ya kwako, ongea namna unavyojisikia, namna kukufuatilia kwake kunavyokuumiza na kukufanya kushindwa kufanya chochote. Usiongee kwa kulia au kulalamika. Hapana ongea kama mwanaume kwa maana ya kuweka hisia pembeni na kuongea kama unaongea dili la biashara vile.

(2) Chunguza Wivu Wake Hasa Nunatokana Na Nini? Katika kuongea naye anaweza asiseme ukweli, kwakua ni mwanaume wakati mwingine anajiona kama ana haki ya kufanya chochote na kukupangia kila kitu hivyo hataona kama ana sababu ya kukupa maelezo yoyote. Unachotakiwa kukifanya ni kuchunguza, kujua kuwa wivu wake unatokana na nini? Mara nyingi wivu wake hata hauhusiani na mambo unayoyafanya bali mambo ambayo anayafanya yeye au jinsi alivyo.

Inawezekana hajiamini kila wakati anahisi utamsaliti anaona hatoshi kwako hivyo anakufuatilia. Inawezekana ni kwakua yeye anachepuka sana hivyo anahisi na wewe unachepuka, lakini wakati mwingine ni kwakua hataki umfuatilie, anakukataza baadhi ya mambo, marafiki na kwenda sehemu kwakua anajua utagundua michepuko yake. Sasa bila kujali sababu hembu chunguza na ujue kama shida ipo upande wako au upande wake, nimuhimu ukajua kwanza kabla ya kufanya chochote.

(3) Badilika Kama Tatizo Ni Wewe; Inawezekana wewe ndiyo unamfanya awe hivyo, mambo ambayo ulikua unafanya kabla au ambayo unayafanya sasa, marafiki zako unaoongozana nao ni wale walioshindikana, wewe hufanyi wanayofanya lakini wao wanafanya, uvaaji wako ni wakutega na unakuonyesha kama uko kibiashara, safari zako za kikazi au hata hapo nyumbani kila wakati ni kuaga nakwenda sehemu flani ha hufiki, simu unazopokea za kificho na meseji unafutafuta, yote haya yanamfanya kuwa na wasiwasi, kama tatizo ni wewe basi acha muambie umeacha na aone umeacha atapunguza na kuacha wivu.

(4) Acha kuwa mtu wa vificho vificho na kujitetea tetea kwa vitu vya kawaida; Kwa wanawake wengi mume au mpenzi anapozidisha wivu basi huanza kuwa wasiri, huanza kudanganya hata wanapofanya mambo ya kawaida. Unataka kutoka na marafiki kupata kinywaji badala ya kumuambia unaona ukimuambia atakasirika uandanganya umeenda kwa Dada yako. Unaweza kudhani kama inasaidia lakini hapana, hiyo ni mbinu ambayo huahirisha tatizo tu lakini akijua ndiyo hatakuamini tena na tena.

Kama hufanyi kitu kibaya huna haja ya kuficha, anapoliza muambie ukweli hata kama akikasirika lakini ajue ni ukweli. Kama kakukataza kuoanana na mtu flani kuliko kudanganya ni bora ukatae afanye la kufanya. Kwamba kama unataka acha kumuona au muone na usifiche, muambie haiwezekani kama haiwezekani na nitafanya kama utafanya. Akikuuliza kitu acha kujitetea sana kana kwamba ni kitu kibaya, jinsi unavyozidi kujitetea kuficha ndiyo unavyozidi kumkasirisha.

Kama ni meseji si lazima ufute kama ni za kawaida, kama ni simu umepigiwa huna haja ya kujificha kama ni marafiki huna haja ya kukutana nao kwa siri. Kila mara unapofanya kitu kwa siri, unapojaribu kujitetea kwa kitu cha kawaida ndiyo unavyozidi kumlisha imani ya kua unachepuka, unazidi kumfanya asikuamini zaidi na zaidi. Fanya mambo kwa uwazi, mwanzoni atakua akikasirika sana lakini baadaye atazoea na kukuamini. Kudanganya mara moja kunaweza kumfanya asikuamini milele.

(5) Msapoti Na Onyesha Upendo Zaidi; Unapoongea na mwenza wako, akakuambia kinachomsumbua, au hakukuambia lakini umejua, unapokua wazi katika kufanya mambo yako, humfichi na humdanganyi niwazi atakua ni mtu wa hasira zaidi. Acha kutaka kuingia kwenye kichwa chake, kumuuliza kama kuna nini na kuomba msamaha kwa vitu ambavyo havina maana au hujafanya. Cha kufanya hapa kama ana hasira wewe ni kuzidisha mapenzi kwake, onyesha kuwa wewe si yule anayekudhania na wala hufanyi yale anayoyaongea.

Kwa kumuonyesha upendo itamuambia mambo mawili, kwanza nikuwa uanmpenda na ni wasiwasi wake tu, lakini pia utakua unamuambia huachi mambo madogo kama yale yaharibu uhusiano wenu. Hapa kuwa makini, usilazimishie mambo, kuna wengine wana hasira hivyo unaweza hata kumgusa akakasirika, chakufanya ni kuacha, kama anaonyesha hasira basi puuza kidogo na usimsogelee sana kwani anaweza hata kukupiga lakini muhimu endelea na maisha yako kama kawaida.

(6) Weka Mipaka Ya Mambo Ambayo Huwezi Kuvumilia; Mwanaume mwenye wivu atataka kucontrol kila kitu katika maisha yako, atataka kukupangia kila kitu. Nimuhimu na nilazima kuweka mipaka kwani kama utamsikiliza kila kitu basi hutakua na maisha na unaweza hata kutamani kujiua kwakua huna furaha. Kwa maana hiyo basi mwanzoni kabisa akionyesha wivu nilazima wewe mwenyewe useme kuwa kitu falani siwezi kufanya, kitu falani siwezi kuacha na ni bora nikose ndoa kuliko kufanya au kuacha hivyo vitu.

Kwa mfano atataka kukuachiasha kazi ili uwe Mama wa nyumbani kataa kwani ukikubali mateso yatakayofuata hutatamani hata hiyo ndoa. Atataka uache kujiendeleza kielimu asifanye biashara ili uwe unamtegemea kwa kila kitu akuthibiti kataa. Anakukataza baadhi ya marafiki, kubali kwa wale unaoona hawana maana kwako lakini si wote, anakukataza kuwasiliana na ndugu zako kataa. Iko hivi kama ukiwa unakubaliana na yeye kila kitu basi atafanya kama mchezo flani.

Kila siku atajisikia tu kukukataza hata kwa vitu vya kijinga, nilazima uwe na mipaka, useme hiki hunikatazi, hiki siwezi kufanyiwa. Useme siwezi kupigwa na nikipigwa ni Polisi kwanza kabla ya kwenda kwa Mshenga na vingine kama hivyo. Bila kuweka mipaka huyo mwanaume atakufanyia makusudi, kila siku ataongeza kitu mpaka atakuambia hakuna hata kutoka ndani na hatafanya hivyo kwa upendo bali kukukomoa tu. Nilazima ajue kua wivu wake unapaswa kuwa na kipimo kwani hata wewe una maisha.

(7) Acha Kumwagia Mbolea Mnuno Wake; Wanaume wengi wenye wivu hasa huu wa kijinga mara nyingi wanapohisi umekosea au bila sababu yoyote ile wanaweza kujinunisha tu, ghafla unaona kama hakuongeleshi au ukimsemesha kanuna. Sasa kama wewe mwanamke unajua hujafanya kosa lolote na umejaribu kuongea naye lakini haeleweki basi hembu acha kuendekeza kununa kwake na endelea na maisha yako kama vile hakuna kilichotokea.

Kwa wanawake wengi ikitokea hivi huanza kuomba msamaha, bila hata kujua kosa huomba msamaha, lakini pia huanza kuuliza kila saa, hivi nimekukosea nini, imekuaje, sijui nini na wasiwasi mwingi. Hapana huyo anafanya kama mtoto aliyedekezwa, hembu kama unaona kuwa hakuna kibaya ulichofanya lakini kajinunisha acha kumundekeza, acha kununa naye, acha kuomba misamaha ya mambo ambayo hata huyajui.

Pata GB 20 Mitandao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz