KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI! - EDUSPORTSTZ

Latest

KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI!


 Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu. Hili ni KOSA KUBWA sana!

Pata GB 10 Mtinadao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona!

Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung’olewe kwanza! Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo.

 Angalia mwenyewe, upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanaume huyu, au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume yule; au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanaume  wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja? Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana.

Nani anaweza kutibu nguvu za kiume?
Kuna watu wengi sana hivi leo wanaodai kutibu nguvu za kiume. Ukweli wa mambo ni kwamba siyo kweli! Ni watu wachache sana wana uwezo wa kutibu tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. 

Utakuta mtu anatangaza dawa ya aina moja kuwatibu watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume. Tabia hii pia imejengeka kwa baadhi ya watu, hupiga simu na kuuliza moja kwa moja, “Daktari, dawa za nguvu za kiume ni shilingi ngapi?”

 Kila mwanamume ana sababu na chanzo chake cha kupungua nguvu za kiume. Kama wanaume 100 waliopungukiwa nguvu za kiume watajipanga mstari, kila mmoja atakuwa na sababu yake na chanzo chake cha kupungukiwa nguvu za kiume tofauti kabisa na mwingine.

Hii humaanisha kila mgonjwa atakuwa na dawa yake ya kipekee kabisa tofauti na mwingine. Sasa itashangaza kuona huyu kapungukiwa nguvu za kiume kutokana na mishipa ya ateri kutofanya kazi vizuri, na yule kapungukiwa nguvu kutokana na kuvimba kwa tezidume,Halafu wote wapate dawa aina moja! Hiki ndicho kinachofanyika na watu wengi wamepoteza pesa na muda kwa matibabu yasiyokuwa na maana.

Yahitajika daktari mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo, ndiye anayeweza kutibu tatizo la nguvu za kiume. Yaani, daktari ambaye anajua vizuri ndani na nje utendaji wa figo, ini, moyo n.k; awe ni daktari wa tiba asilia au daktari wa tibakemikali (yaani daktari wa hospitali) siyo kila mtu tu au kila daktari. 

Pata GB 10 Mtinadao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Hata kama utakwenda kwenye hospitali kubwa yoyote duniani unayoijua, na ukagonga hodi katika chumba cha daktari, ukamwambia, “Nina tatizo la upungufu au kuishiwa nguvu za kiume,” atakurifaa kwa daktari maalumu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo. 

Hata kwa madaktari wa tiba asilia, hali ni hivyo hivyo, lazima ukutane na ambaye amebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Kwa sababu unapotibu nguvu za kiume unakuwa unatibu viungo vya mwili kwa ujumla. Daktari aliye mtaalamu anakuwa ana uwezo wa kutambua tatizo la kiungo kilichokorofisha mwilini kutokana na kumhoji mgonjwa; na anaweza kwenda mbali zaidi kwa kujiridhisha kwa vipimo.

Pata GB 10 Mtinadao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz