SABABU Zinazoweza Kupelekea Mwanamke Asiolewe Kabisa - EDUSPORTSTZ

Latest

SABABU Zinazoweza Kupelekea Mwanamke Asiolewe Kabisa

SABABU Zinazoweza Kupelekea Mwanamke Asiolewe Kabisa

Kuoa au kuolewa ni jambo ambalo watu wengi hutamani kwani ni miongoni mwa hatua kubwa  katika maisha ya kila mmoja. Ukifanya utafiti kwa watu ambao hawajaoa wengi watakwambia wanatamani siku moja wawe na familia bora na yenye furaha, kwani kila mmoja anaamini hayo ni mafanikio kwenye maisha.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Licha ya kuwa kuolewa au kuoa ni jambo jema, baadhi ya watu huwa hawaoi au hawaolewi. Kuto kuoa au kuolewa kunaweza kuelezewa na sababu nyingi sana. Leo tutazungumzia suala la mwanamke kuolewa, na tutaweka bayana baadhi ya tabia chache ambazo zinaweza (zinachangia kwa kiasi kikubwa) mwanamke kuto kuolewa.

Utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii- Hili najua si kwa wanawake tu, lakini kwa sababu leo wao ni walengwa wa mada, tutazungumzia upande wao tu. Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao  ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, wakiinua macho basi wanaangalia Tv na akimaliza channel hii atahamia nyingine, akimaliza mtandao huu atahamia mwingine. Kutwa nzima unakuta anafuatilia staa huyu alifanya nini usiku, huyu alipiga picha gani, kikapanda kikashuka.

Soma Zaidi>>> Sammata : Siondoki Astonvilla

Mwisho wa siku mwanamke kama huyu atakuwa hana cha maana alichojifunza kwenye mitandao au kutazama Tv zaidi ya kuanza kuiga yale aliyoyaona. Na hakuna mwanaume muoaji anayetaka mwanamke ambaye akili yake imetawaliwa na mitandao ya kijamii hakumbuki hata kufanya usafi ndani.

Kutokupenda kufanya kazi za nyumbani- Wanawake wengi wa ki-Afrika kwa vile wamekwenda shule wakatambua mambo ya haki sawa kwa wote na wengine kuona kwenye filamu wanaume wakifanya kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake, basi na wao ndio wameweka nukta kufanya kazi za nyumbani.

Kuto kana na hali hii, wanawake wamekua wakujiremba tangu mawio hadi machweo, ukitazama kucha zao zilivyondefu unajiuliza hutu anafua kweli? wengine wame amua kuajiri watu wa kuwafulia hadi nguo za ndani. Kwa hali hii isitarajie mwanaume akuoe kwa sababu anajua ni matatizo anapeleka nyumbani.

Soma Zaidi>>> Azam Fc Watamba Wapo Fiti Kiwanis Ubingwa

Kujipara hadi sura yako ya asili inasahaulika- Ni kweli wanaume hupenda mwanamke mrembo na mwenye kupendeza. Lakini hii haimaanishi ndio ujipodoe hadi uchukize. Kila kitu  kwa kiasi chake kwa sababu kitu chochote kikizidi huwa ni sumu.

Jirembe kwa kiasi, hili litavutia watu walio-serious kutaka kukuoa, lakini ukiwa ni wa kujiremba hadi ukapindukia, hakuna muoaji atakaye kuta. Tena ikumbukwe kuna baadhi ya wanaume wao hupenda mwanamke asiyejiremba (wenyewe huita natural)

Hizi ni baadhi tu, na wewe unaweza kuongezea ili kuwakumbusha wasichana wanaotaka kuolewa.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz