Njia Zitakazowasiaidia Muweze Kudumu Katika Mahusiano Yenu ya Kimapenzi - EDUSPORTSTZ

Latest

Njia Zitakazowasiaidia Muweze Kudumu Katika Mahusiano Yenu ya Kimapenzi


 Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa pia. Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na mtakapoishi.

1. Kuwa na muonekano chanya kwa mpenzi wako.
Ukiwa ni mtu wa kuangalia mabaya/kasoro sana kwa mpenzi wako kuliko mazuri yake hautakuja kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu hata siku moja, utaendelea kubadilisha wanaume/Wanawake kila siku na mwisho wa siku utajiona huna bahati kwenye mapenzi na wakati Unayeyaharibu mapenzi yako ni wewe Mwenyewe…kakuna asiye na kasoro (ukiwemo wewe mwenyewe).

Kwa hiyo muonyeshe mpenzi wako mapenzi bora na umrekebishe pale anapokosea Bila kuwa na lawama mara kwa mara, kuna makosa mengine ni hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in return. Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

2. Mpe nafasi na uhuru mpenzi wako.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na kimaisha. Anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo yake. Usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.

Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.

3. Mfanye mwenza wako ajivunie kuwa nawe kila wakati.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye.

Wapo wengi sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua. Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.

4. Msadie kwa hali na mali kila inapowezekana.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na kushuka miongoni mwa wapenzi na hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika hali ambayo hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote hakikisha wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi.Sio matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo chanya inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe. Kama unampenda usione tabu kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa hiyo jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na mpenzi wake.

Yapo mambo mengi sana ambayo kama mkiyafanya kwenye mapenzi basi uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha sana ingawa hapa nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia sana kwa wote walio kwenye mahusiano .

Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku moja, unapoona wapenzi wengi wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu wanavumiliana kwa mengi na kusameheana kwa mengi. sana na unaweza kuyarekebisha kwa kukaa chini na mpenzi wako mkayamaliza kwa dakika 5 tu lakini wengine huwa issue kubwa kwao na kusababisha mwisho mbaya.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz