JE, NI SAHIHI KUOMBA USHAURI KWA MTU MWINGINE JUU YA MASUALA YAKO YA MAPENZI? - EDUSPORTSTZ

Latest

JE, NI SAHIHI KUOMBA USHAURI KWA MTU MWINGINE JUU YA MASUALA YAKO YA MAPENZI?


 MPAKA leo kuna baadhi wana swali kuhusiana na suala hili. Wapo wanaoamini ni sahihi na wapo wanaoamini si sahihi.

Wanaoamini si sahihi wanaonekana kuwa na hoja pana kiasi kwa upande wao. Mmoja niliwahi kumsikia akisema:

“Kumshirikisha mtu baki katika uhusiano wako ni kama kumdhalilisha mtu wako, maana kama unashindwa wewe kumuweka sawa ni kwa namna gani mwingine amuweke sawa,” akaendelea!

“Kwanza unapokuwa na tabia ya kuongea masuala ya mpenzi wako kwa mtu mwingine, unashusha ile heshima na hadhi yako katika uhusiano.

Eti mwanaume mzima umewekwa chini na mwanaume mwenzako anakwambia cha kufanya kwa mkeo, hii hi haki kweli?

Tena hii inaweza kusababisha hata uhusiano wako ukazidi kuyumba kwa maana unayemwambia anaweza kutumia udhaifu wako kumteka mpenzi wako’’, tuishie kwanza hapo.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Wapo wanaosema mengi zaidi ya hayo, ila kwa maneno hayo atakuwa kawakilisha wengi. Wewe unaamini nini katika uhusiano wako? Ni haki kuyasema matatizo yako kwa mwingine katika lengo la kutafuta suluhu au ni vyema kukaa nayo ‘moyoni’ hata kama mmeshindwa kupata ufafanuzi?

Ni vyema ikaeleweka kuwa kunapotokea tatizo ni vyema likatafutiwa ufumbuzi mapema na hatimaye kutatuka. Kama kuna tatizo na hakuna ufumbuzi, basi tatizo husika litadumaza akili za wahusika na kusababisha waanze kutafsiriana tofauti.

Kitaalamu, kumweleza mtu tatizo lako hata kama hajalitatua kimantiki, ila huwa inaleta faraja katika akili na aina fulani ya ahueni katika hisia za mhusika.

Kukaa na tatizo baada ya kushindwa kulimaliza wenyewe na kuogopa kuwahusiha watu wengine kwa imani kuwa si sahihi ni njia ya kutaka kuyaingiza mahusiano yako katika hali ngumu zaidi.

Mfano, unahisi mpenzi wako anakusaliti baada ya kuona dalili fulani, ila baada ya kumuuliza juu ya suala hilo akakanusha. Na katika ukanushi wake hajakushawishi kuamini kwa dhati kuwa hakusaliti, hivyo ukabaki kuendelea kuamini kuwa anakusaliti. Katika hali hii ukikaa na suala husika katika nafsi yako matokeo yake ni nini?

Ni vyema kuwa na utaratibu wa kuomba ushauri kwa masuala ambayo unahisi yamekushinda. Ushauri maana yake sio hujui kitu! Hapana. Ila kitalaamu, mtu anapokuwa na tatizo uwezo wake wa akili katika kufanya kazi hupungua kutokana na muda mwingi kuwaza tatizo husika badala ya kuwaza namna ya kutatua. Kwa hali hiyo, mtu wa aina hii anahitaji kufundishwa kitu au kukumbushwa jambo la kufanya.

Unaweza kwenda kwa mtu yeyote mwenye hekima na busara unayeona anafaa kuombwa ushauri. Au kama unahisi suala hili linahitaji maelezo na maneno ya ziada wapo washauri wa masuala ya saikolojia ya mahusiano. Wanaweza kukusaidia na hatimaye mahusiano yako yakaleta amani na furaha.

Acha kuogopa kuomba ushauri kwa masuala yako ya kimahusiano. Kama kuna tatizo omba ushauri, tafuta namna ya kujua kitu usichokijua vizuri, omba mtu akukumbushe jambo ambalo huenda umelisahau.

Ushauri ni njia ya kuiweka akili yako katika hali nzuri ya kupambana na changamoto za uhusiano wako. Baada ya mhusika kukwambia nini unatakiwa kufanya utaona akili yako inavyofunguka na kujua ni nini hasa unatakiwa kufanya au kutenda.

Ushauri stahiki ni moja kati ya njia za kuleta amani na utulivu katika uhusiano wako. Kwanini usiutake? Omba ushauri kwa kila jambo unalohisi hulielewi vizuri.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz