SAUTI INA RAHA YAKE KWENYE MAPENZI - EDUSPORTSTZ

Latest

SAUTI INA RAHA YAKE KWENYE MAPENZI


Sauti Siku Zote Ina Maana Kubwa Sana Katika Mtiririko Wa Wewe Kujua Mwenzako Ana Maanisha Nini.Sauti Vilevile Inaweza Kukupa Picha  Jinsi Alivyo Kutegemeana Na Ongea Yake.Sauti Huwezesha Lugha Yako Unayoiwasilisha Kueleweka Vizuri Kwa Msikilizaji Endapo Utaitumia Ipasavyo.

Je wajua sauti ya mtu kwa harakaharaka inamtambulishaje kwa msikilizaji?

• Mpole

• Mkali

• Hekima na busara au

• Hasira

Linapokuja suala la mahusiano,ni vizuri uzingatie matumizi ya sauti kutegemeana na muda na hali Fulani ya maongezi.

Pale  mnapokoseana, ni vizuri ukatumia sauti yako kumshusha mwingine ili muweze kufikia muafaka.Ukiendeleza sauti ya ukali hatakama haumaanishi kubishana, si rahisi kufikia muafaka sanasana mtaishilia kuchukizana zaidi.

Sauti hutumika katika kubembeleza ,yale mahadhi yakupanda na kushuka kwa sauti yako humjengea mtu hisia na ladha Fulani tofauti na unapokua katika maongezi ya kawaida au ya wewe na rafiki yako.

Unapokua na mpenzio hakikisha unatumia sauti yako ipasavyo katika kunakshi maongezi yenu na kuyafanya yawape furaha nakuwa na hamasa zaidi ya muendelezo wa mazungumzo au shughuli nyingine bila kuchoka.

Siimaanishi uige sauti ya Fulani,hapana.Bali kuwa mbunifu wa utumiaji wa sauti yako.

Kuwa miongoni ya wale ambao wanapendwa kusikilizwa na wapenzi wao,sio kwa ajili ya mapenzi ya dhati tu ,bali kwa jinsi wanavyoteka nafsi ya mwenziwe kwa matumizi mazuri ya sauti yanayoipamba lugha na maongezi kwa ujumla.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz